Kundi la Wanaharakati Wasiojulikana limekuwa likiishambulia Urusi mtandaoni tangu lilipotangaza "vita vya kimtandao" dhidi ya Rais Vladimir Putin ili kulipiza kisasi uvamizi wa Ukraine.Watu kadhaa wanaoendesha shughuli zao kwa ushirikiano na kundi hilo wamezungumza na BBC kuhusu nia, mbinu na mipango yao.
Kati ya mashambulio yote ya kimtandao yaliyofanywa tangu kuanza kwa mzozo wa Ukraine, udukuzi watu wasiojulikana dhidi ya mtandao wa Televisheni ya Urusi imesalia kuwa juu.
Udukuzi huo ulinaswa katika vido fupi ambayo inaonyesha jinsi matangazo ya kawaida yalivyokatizwa kwa picha za mabomu yanayolipuka Ukraine na wanajeshi wanaozungumza kuhusu jinamizi la mzozo huo.
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Video hiyo ilianza kusambaa mitandaoni mnamo Februari 26 na ilishirikishwa na akaunti za mtandao wa kijamii wa Anonymous zilizo na mamilioni ya wafuasi. "YANAYOJIRI HIVI SASA: # Vituo vya Televisheni nchini Urusi vimedukuliwa na #Anonymous kutangaza ukweli kuhusu kile kinachofanyika ndani ya #Ukraine," ujumbe mmoja ulisema.
Video hiyo ilitazamwa na mamilioni ya watu ndani ya muda mfupi.
Tukio hili lina ishara zote za udukuzi usiojulikana - wa ajabu, wenye athari na rahisi kushirikisha mtandaoni. Sawa na mashambulizi mengine mengi ya kimtandao ya kundi hilo pia ilvyoikuwa vigumu sana kuthibitisha.
Lakini moja ya vikundi vidogo vya wadukuzi wasiojulikana walisema kwamba waliwajibika, na kwamba walichukua huduma za TV kwa dakika 12.
Mtu wa kwanza kuweka mtandaoni video hiyo pia aliweza kuthibitisha kuwa ni kweli. Eliza anaishi Marekani lakini babake ni Mrusi na alimpigia simu wakati vipindi vya televisheni vilikatizwa. "Baba yangu alinipigia simu na kusema, 'Oh Mungu wangu, wanaonyesha ukweli!' Kwa hivyo nilimuomba airekodi na ndipo nikaweka kipande hicho mtandaoni. Anasema rafiki yake mmoja aliona pia.
Rostelecom, kampuni ya Kirusi inayoendesha huduma za udukuzi haikujibu ombi letu la kutoa maoni juu ya suala hilo.
Wadukuzi hao walihalalisha vitendo vyao wakisema raia wa Ukraine wasio na hatia walikuwa wakiuawa kinyama. "Tutazidisha mashambulizi dhidi ya Kremlin, ikiwa hakuna kitakachofanyika kurejesha amani nchini Ukraine," waliongeza.
Anonymous pia inasema iliondoa tovuti za Urusi na kuiba data za serikali, lakini Lisa Forte, mshirika wa kampuni ya Red Goat - ya usalama wa mtandao anasema mashambulizi hayo hayana ''msingi wowote".
Wadukuzi wamekuwa wakitumia mashambulizi ya DDoS, ambapo seva inatumiwa maombi mengi kupita kiasa, alisema. Haya ni rahisi kutekeleza na huathiri tovuti nje ya mtandao kwa muda tu.
"Lakini udukuzi wa runinga ni wa ubunifu wa hali ya juu," alisema,
Anonymous ni kina nani?
- Kundi la wanaharakati hao liliibuka kwa mara ya kwanza mwaka wa 2003 kutoka kwa tovuti ya 4chan
- Kundi hilo halina uongozi, kaulimbiu yake ni "Sisi ni jeshi"
- Mtu yeyote anaweza kudai kuwa sehemu ya kundihilo na kudukua kwa sababu yoyote anayotaka, lakini kwa ujumla washiriki hushambulia mashirika yanayotuhumiwa kutumia mamlaka vibaya.
- Nembo yao ni ni mtu aliyevalia barakoa, maarufu iliyotokana na mchoro wa kitabu cha V kwa maana ya uhasama ambamo mwanamapinduzi asiye na sheria anapindua serikali ya kimabavu.
- Kundi hilo lina akaunti nyingi za mitandao ya kijamii, iliyo na wafuatiliaji milioni 15.5 katika kurasa zake za Twitter pekee.
Wadukuzi wasiojulikana pia wameharibu tovuti za Kirusi. Forte anasema hii inahusisha kupata udhibiti wa tovuti ili kubadilisha maudhui yanayoonyeshwa.
Kufikia sasa, mashambulizi hayo yamesababisha usumbufu na aibu, lakini wataalam wa mtandao wameshangazwa na mlipuko wa wanaharakati wa shambulio la kimtandao tangu uvamizi wa Ukraine.
Wna wasi wasi kuwa wadukuzi hao huenda wakashambulia mtandao wa kompyuta za hospitali au kuvuruga mawasiliano ya muhimu.
"Sijawahi kuona kitu kama hiki," anasema Emily Taylor wa jarida la Cyber Policy.
"Haya mashambulio ni hatari. [yanaweza] kuzongezeka, au mtu anaweza kuathiri sehemu muhimu ya maisha ya kila siku ya raia."
Anonymous haijakuwa ikihudumu kwa miaka kadhaa. Roman, mfanyabiashara wa teknolojia wa Ukraine nmbaye anaongoza kundi la wadukuzi linaloitwa Simama na Ukraine, hakuwa na uhusiano wowote na shirika hilo hadi Urusi ilipovamia nchi yake.
Lakini ameiambia BBC kuwa yeye na wanzake waliharibu kwa uda tovuti ya shirikala la habari la Urusi, Tass, na kuweka picha inayomkashifu Putina na nembo ya wadukuzi wasiojulikana.
Roman anafanya kazi mjini Kyiv, ambako amekuwa akiongoza wafanyakazi wake kuunda tovuti, programu za Android na roboti za Telegram ili kusaidia juhudi za vita vya Ukrainia, na kudukuaasasi muhimu ya Urusi.
"Niko tayari kuchukua silaha kupigania Ukraine, alikini kwa sasa ujuzi wangu unatumika vizuri kwenye kompyuta. Kwa hivyo niko hapa nyumbani kwangu na kompyuta zangu mbili, nikiratibu upinzani huu wa kiteknolojia."
Anasema kundi lake liliduku na kuondoa huduma ya tikiti ya treni ya eneo la Urusi nje ya mtandao kwa saa kadhaa, ingawa BBC haijaweza kuthibitisha hili..
Anatetea matendo yake akisema: "Mambo haya ni haramu na ni makosa mpaka kuwe na tishio kwako au kwa jamaa zako."
Kundi lingine ambalo limeunganishwa na Anonymous ni timu ya wadukuzi wa Kipolandi inayoitwa Squad 303, iliyopewa jina la kikosi maarufu cha wapiganaji wa Poland katika Vita vya Pili vya Dunia.
No comments:
Post a Comment