Msichana akuza nywele zake kwa miaka ili kuchangia wahitaji - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday 22 March 2022

Msichana akuza nywele zake kwa miaka ili kuchangia wahitaji

 

m

CHANZO CHA PICHA,FAMILY PHOTOS

Poppy Lee-Burrowes ana umri wa miaka 11 tu, lakini amekuwa akikuza nywele zake katika maisha yake, kwa malengo.

Alipokuwa na umri wa miaka 5, amekuwa akitaka kutoa nywele zake kwa shirika la kusaidia wahitaji la The Little Princess Trust, lililopo nchini Uingereza ambalo hutoa nywele asilia bila malipo kwa watoto na vijana ambao wamepoteza nywele zao kufuatia matibabu ya saratani au kwa sababu nyingine.

Maelezo ya sauti,

Nywele ndefu zampatia mtoto mvulana umaarufu mitandaoni

Lakini Poppy alikutana na shida.

Nywele zake ni laini sana, na watengeneza wigi walikuwa wametoa angalizo kwamba wasingeweza kuzitumia kwa sababu zinakatika kwa urahisi.

Ushonaji wa wigi la asili unaweza kuchukua kati ya saa thelathini na sitini, na wakati mwingine huhitaji nywele za watu 12 hadi 14 .

"Little Princess Trust" ilizalisha wigi za Afro, lakini kwa nywele za Ulaya, ambazo zenye kujiviringa.

Michango kutoka kwa watu weusi na mchanganyiko ilipunguzwa kwa sababu ya udhaifu wa nywele.

Poppy na mama yake walianza kuchangisha pesa na kukusanya zaidi ya Dola za Marekani 3,500.

Ndoto imetimia

Hatimaye, mbinu iliyotengenezwa mwaka 2021 ilimruhusu Poppy kutimiza ndoto yake.

Njia iliyo katika swali inalinda nywele na kuhakikisha uimara wake wa kukaa muda mrefu, ambayo ina maana kwamba kituo hicho sasa kinaweza kukubali nywele za afro.

"Ninajisikia furaha sana na kichwa changu ni chepesi sana. Natumani hii itawatia moyo watu wengine kuchangia pesa na nywele zao," alisema.

"Ninajivunia sana nilichofanya. Ni muhimu kuchangia nywele za Afro kwa sababu ni sehemu muhimu ya utambulisho wa watu wengi," aliongeza.

Phil Brace, mtendaji mkuu wa 'Little Princess Trust', alisema 'uwepo wa vijana kama Poppy unatia moyo na kufurahisha'.

m

"Siku zote ilikuwa changamoto kwa sababu ni afadhali tusifanye wigi hizi. Vijana tayari wanakabiliana na changamoto ya kupoteza nywele zao, na hiyo ni juu ya wasiwasi wa kama watapata wigi inayofaa zaidi," anaongeza Brace.

Beki Lee-Burrowes, mama wa msichana huyo, alisema kwamba "kujua kwamba mtoto ambaye anaugua saratani, ambaye anapitia wakati mgumu katika maisha yake, anapata nywele zinazowafaa ni zawadi kubwa kwao" .

Lakini huo sio mwisho wa simulizi ya Poppy, ambaye anasema yuko tayari kuruhusu nywele zake kukua na kuchangia tena. "Nataka kuzitunza tena ili nichangie siku zijazo," alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here