Tangazo: wanajeshi wa zamani walio na uwezo wa kuzungumza lugha tofauti na walio tayari kwenda Ukraine kisiri kwa kipato kizuru cha hadi $2,000 (£1,523) kwa siku na - marupurupu ya ziada - kusaidia katika uokozi wa familia kutokana na mzozo unaozidi kuwa mbaya.
Inaonekana kana kwamba limetolewa kwenye hati ya filamu ya kama sehemu ya vita, lakini ni tangazo halisi la kazi - lilichapishwa katika tovuti ya ajira linalofahamika kama, Silent Professionals, kwa wale wanaofanya kazi katika sekta ya kijeshi na usalama wa kibinafsi.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA:Kwanini Marekani inaogopa kuzituma ndege za Poland kwenda Ukraine?
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Na, wahusika wa ndani wanasema, hitaji linaongezeka.Huku kukiwa na vita vikali nchini Ukraine,wakandarasi wa kibinafsi wa Maekani na Ulaya wanasema wazidi kutazamia fursa , kuanzia oparesheni ya uokozi hadi kusaidia na vifaa vingine muhimu.
Leo hii kuna "hitaji kubwa katia soko" la wakandarasi wa kibinafsi nchini Ukraine, alisema Robert Young Pelton, mwandishi wa Marekani mzaliwa wa Canada na mtaalamu wa makampuni ya kijeshi ya kibinafsi (PMCs).
Lakini mahitaji ta wafanyakazi wa usalama wa kulipwa - wengi wao wakiwa wanajeshi wa zamani wenye uwezo wa kupigana na kuua- vitani hutoa nafasi kubwa ya makosa mbayo huenda yakazua hali ya mtafaruku na kuchangachinkiwa.
Hata wafanyakazi wa kujitolea kutoka nchi za Magharibi wanajiunga na vita vya Ukraine,wanatarajia kulipwa sawa na wenzao wa Ukraine, na pesa zinatolewa na watu wenye maslahi ya kibinafsi katika huduma za usalama kama zile zinazotangazwa katika tovuti ya Silent Professionals.
Jukwaa hilo la ajira halitaji anayetoa tangazo ni nani, lakini kulingana na Bw. Pelton, wakandarasi wanaajiri kwa kati ya $30,000 na $6m kusaidia kuondoa watu Ukraine. Kiwango cha juu cha malipo hayo ni cha kundi zila la familia inayotaka kuondoka na mali yao,alisema.
Ada ya kuondoa watu inategemea ugumu wa kazi, alisemaTony Schiena, Afisa Mkuu Mtendaji wa Mosaic, kampuni ya ushauri wa kijasusi yenye makao yake makuu Marekani na ambayo tayari inafanya kazi nchini Ukraine.
"Wakati kuna kundi kubwa la watu, hatari inaongezeka. Watoto na familia wanapokuwa ni vugumu zaidi. Yote inategemea mbinu ya kuwafikisha upande wa pili".
Paresheni ya Mosaic sana sana hutegemea ujasusi, bada ya silaha, alisema Bw.said Schiena, mafanyakazi wa zamani wa kijasusi ambaye kampuni yake inajumuisha maafisa wa zamani wa kijasusu wa ngazi ya juu wa Marekani kwenye bodi yake.
Wanafanya kazi na wateja wa kibinafsi, mashirika na PIPs -watu waliowekwa wazi kisiasa- kusaidia kuwahamisha kutoka Ukraine, Bw. Schiena aliambia BBC.
Anadai "shirika la kijasusi la nchi kubwa" inayotaka kuondoa raia wake nchini humo ni miongoni mwa wateja wake..
"Kulingana na jinsi mzozo utakavyokuwa, Nafikiria kutakuwa na hitaji la mara kwa mara [PMCs]," Bw. Schiena alisema. "Kuna hitaji la mara kwa mara, na [vita] vinapoongezeka au kupungua, daima kutakuwa na kitu ambacho tunakaribia kufanya".
Mashirika ya kibinafsi ya kijeshi na usalama yamekuwepo kwa miongo kadhaa, lakini yaliwekwa hadharani wakati wa vita vya Iraq na Afghanistan baada ya shambulio la9/11, yakifanya kazi kwa niaba ya serikali za Magharibi na masilahi ya kibiashara.
Katika kilele cha vita vya Iraq, maelfu ya wakandarasi binafsi, kama vile Blackwater, walikuwa wakifanya kazi huko. Majukumu yao yalijumuisha ulinzi wa msafara hadi malisho na makazi ya wanajeshi katika kambi za kijeshi. Blackwater ilijulikana sana baada ya matukio kadhaa makubwa, ikiwa ni pamoja na vifo vya raia 14 wa Iraqi waliouawa kwa kupigwa risasi na wakandarasi wake huko Baghdad mnamo 2007.
Ulaya Mashariki, makampuni ya kibinafsi ya usalama yametumiwa kwa muda mrefu kulinda watu matajiri na mashirika.
Wakati wa kuvunjika kwa Yugoslavia ya zamani, makampuni kadhaa pia yaliajiriwa kusaidia kuandaa, kutoa mafunzo na kupanga vikosi vya Bosnia na Kroatia - yote kwa baraka za serikali ya Marekani.
Asili ya tasnia inamaanisha kuwa kufuatilia idadi ya kandarasi na pesa ni ngumu, lakini kwa kila hali ni tasnia inayokua. Ripoti kutoka Aerospace & Defense News iligundua kuwa sekta ya kijeshi na usalama wa kibinafsi duniani itakuwa na thamani ya zaidi ya $457bn (£348bn) mwaka 2030, kutoka takriban $224bn mwaka wa 2020.
Wakandarasi au mamluki?
Wakandarasi wa kijeshi wa kigeni wanasema hawapigani nchini Ukraine.
Baadhi wanasema wanaombwa usaidizi na mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya misaada ya kibinadamu nchini Ukraine au nchi jirani zinazohitaji watu wenye ujuzi maalumu na uzoefu wa kufanya kazi katika mazingira magumu katika maeneo yenye migogoro.
"Wengi wa vijana ninaowatuma ni madaktari, wasaidizi wa madaktari, wahudumu wa afya, wauguzi na wahudumu maalum wa zamani - au askari wasio maalum - ambao ni madaktari wa vitatani na wanaelewa," alisema Mykel Hawke, afisa wa zamani wa kikosi maalum cha Marekani. ambaye amefanya kazi kama mkandarasi wa eneo la vita.
Wakandarasi wa Magharibi wanaongozwa na sheria na kanuni za nchi zao wenyewe, alisema Christopher Mayer, Kanali wa zamani wa Jeshi la Marekani ambaye alifanya kazi na PMCs nchini Iraq.
Wanatakiwa kuwalinda watu, mahali au mali,badala ya kushiriki moja kwa moja vitani.
Baadhi ya watu katika tasnia hiyo hushangazwa na dhana kwamba wao ni 'mamluki' au askari wa ziada.
"Ni aina ile ile ya kazi unayoiona Marekani na kwingineko," Bw Mayer alisema. "Tofauti ni kwamba katika maeneo yenye migogoro, uwezekano wa kutumia nguvu kupita kiasi ni mkubwa zaidi".
Mifano ya makampuni kama hayo kuchukua mtazamo wa kivita katika migogoro ni pamoja na Executive Outcomes yenye makao yake makuu Afrika Kusini, ambayo lipigana kwa niaba ya serikali ya Angola na Sierra Leone katika miaka ya 1990.
Sandline International, yenye makao yake makuu jijini London, lilihusika na mizozoz katika mataifa ya Papua New Guinea, Liberia na Sierra Leone.
Na wanachama wa kundi la mamluki wa Urusi wanasemekana tayari wako nchini Ukraine.
Lakini Simon Mann, aliyekuwa afisa wa kikosi maalum cha Uingereza na mwanzilishi wa Executive Outcomes na Sandline, aliambia BBC kwamba matarajio ya kutumia wanakandarasi wa Magharibi kwa oparesheni ya kivita nchini Ukraine "ni magumu" na yataleta maswali magumu ya kisheria na upangaji.
Je [watafadhiliwa vipi]? Je [wataelekezwa] vipi? Watajumuishwa wapi katika mpangilio wa vita vya Ukraine?" aliuliza. "Je, wangesajiliwa ipasavyo katika jeshi la taifa kabla ya operesheni yoyote? Ikiwa sivyo, basi wana nafasi gani kisheria? Majeruhi? Bima ya matibabu? Bima ya kifo na ulemavu?"
Bw Mann - ambaye alifungewa gerezani kwa miaka kadhaa baada ya kushutumiwa kwa kuongoza mapinduzi ya serikali ya Equatorial Guinea mwaka 2004- hata hivyo, alisema kuwa anafahamu juu oparesheni za uokoaji zinazotoza pauni 10,000 kwa kila mtu, "zaidi zikipangwa na watu wa aina ya PMC ambao hutokea kuwa na mawasiliano mashinani"
Baadhi wameonya kuwa hata oparesheni za uokoaji za kulipia nchini Ukraine zinaweza kuwa hatari kwa walinda usalama wa kibinafsi na wateja, na kwamba sekta hiyo imevamiwa na watu wanaowakilisha visivyo uwezo au uzoefu wao.
No comments:
Post a Comment