Mshambuliaji wa Manchester United na Ureno Cristiano Ronaldo, 37, amefanya mazungumzo na wakala wake Jorge Mendes kuhusu hatma yake Old Trafford. (Sun)
Mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland wa miaka 33- Robert Lewandowski ananyatiwa na Manchester United. (Bild - in German)
Mkufunzi wa Aston Villa Steven Gerrard anataka klabu hiyo kutekeleza chaguo lao la kumsajili Philippe Coutinho kwa euro 40m (£33.5m). Hata hivyo, Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye amefanya vyema wakati wa uhamisho wake wa mkopo kutoka Barcelona, lazima apunguze mshahara wake wa pauni 480,000 kwa wiki ili kujiunga na klabu hiyo ya Ligi ya Primia. (Telegraph - subscription required)
Villa huenda pia wakamlenga kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips ikiwa Leeds wataondolewa kwenye michuano hiyo. Bodi ya Villa imejadili ununuzi wa mchezaji huyo wa miaka 26- na timu ya kumsajili inamtaka sana. (Athletic - subscription required)
Juventus wanajianda kuamua ikiwa watamrefushia mkataba mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 28, au kushinikiza kumrejesha kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba katika klabu baada ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kwa Manchester United mnamo 2016.(Tuttosport - in Italian)
Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel ametoa wito kwa mlinzi wa Denmark Andreas Christensen, 25, kupuuza Barcelona na kubakia Stamford Bridge. (Mirror)
Beki wa Uingereza Luke Shaw, 26, anapania kutia Saini mkataba mpya Manchester United. (90min)
Arsenal wamepatia kipaumbele mpango wa kuwasajili washambuliaji wawili na kiungo wa kati mmoja kama sehemu ya kuimarisha kikosi chao msimu huu wa joto. Gunners pia huenda wakamnunua winga mpya na mabeki wawili may also target a new winger, left-sided centre-back and right-back. (Standard)
Sevilla wameongeza kipengele cha kutolewa kwa Diego Carlos hadi euro milioni 80 (£67m). Newcastle ilijaribu kumsajili Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 28 mwezi Januari lakini timu hiyo ya Uhispania haikuwa tayari kumuuza beki huyo. (Goal)
Atletico Madrid wanaongoza katika mbio za kumsajili kiungo mahiri wa Ufaransa na Marseille Boubacar Kamara. Manchester United na Newcastle pia wamehusishwa na uhamiso wa mchezaji huyo wa miaka 22- lakini Atletico wanapewa nafasi kubwa ya kupata. Huduma yake kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (Footmercato - kwa Kifaransa)
Winga wa Uhispania Bryan Gil, 21, anaweza kusalia Valencia msimu ujao baada ya kujiunga na klabu hiyi kwa mkopo Tottenham mwezi Januari. (Star)
Kiungo wa Uholanzo Ryan Gravenberch, 19, yuko tayari kujiunga na Barcelona kutoka Ajax msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)
No comments:
Post a Comment