Katika vita wapo wenye wasiwasi, wengine wanaogopa, lakini kuna maelfu ya raia wa Ukraine ambao wameamua kujiunga na vikosi na jeshi lao kuilinda nchi yao dhidi ya uvamizi wa Urusi ulioamriwa na Vladimir Putin mnamo Februari 24.
Wananchi kutoka asili karibu wameitikia wito wa serikali ya Kiev, ambayo ina nguvu ya kijeshi na idadi ndogo ya watu kuliko ile ya Urusi.
Wengine wameamua kutumia 'Molotov cocktails' haya ni mabomu ya nyumbani yaliyotengenezwa kwa vitu vinavyoweza kuwaka na kuwekwa kwenye chupa.
Picha za watu wa kawaida waliojitolea kusaidia kuelekeza kuhusu utengenezaji wa mabomu haya ya nyumbani zimesambaa duniani kote.Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
Mbali na mabomu hayo, pamoja na silaha nyingine walizokabidhiwa na serikali, raia wamesaidia miji mikubwa ya Ukraine, kama vile Kiev au Kharkiv, ikibaki chini ya udhibiti wao.
Wizara ya Ulinzi hata iliweza hata kuwaongoza kwenye mitandao yao ya kijamii namna ya kuzitumia dhidi ya magari ya jeshi la Urusi.
Jina la "mabomu haya ya nyumbani" linatokana na heshima ya zamani ya Umoja wa Jamhuri za Kisoshalisti za Soviet (USSR), Vyacheslav Mikhailovich Molotov, ambaye alikuwa mhusika mkuu wa mgogoro mwingine wa kijeshi.
Vyacheslav Mikhailovich Molotov alikuwa nani?
Vyacheslav Mikhailovich Molotov, raia wa Urusi aliyezaliwa na jina la Scriabin, alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa USSR mara mbili, kati ya 1939-1949 na 1953-1956.
Alizaliwa mwaka 1890 kutoka kwa wazazi wa tabaka la kati, kuanzia 1906 alikuwa sehemu ya kikundi cha Bolshevik cha Chama cha Kidemokrasia cha Jamii cha Kirusi, ambacho baadaye kikawa Chama cha Kikomunisti cha USSR.
Kwa mujibu wa Kituo cha Wilson nchini Marekani, alikuwa mshirika wa Vladimir Lenin na Joseph Stalin katika mapinduzi ya 1917, ambayo yalisababisha kuanguka kwa Tsarist dynasty na kutoa njia kwa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Urusi ya Federative.
Baadaye, alishika nyadhifa mbalimbali katika chama, kama vile katibu wa Kamati Kuu na uongozi wa Kamati ya Chama huko Moscow.
Mkataba wa Molotov-Ribbentrop
Hata hivyo, anajulikana zaidi kwa kusaini - kama kamishna wa mambo ya nje - mkataba wa Molotov-Ribbentrop mnamo Agosti 1939, mkataba wa amani kati ya USSR ya Stalin na Ujerumani ya Nazi ya Adolf Hitler.
Mkataba huo, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, pia ulikuwa na makubaliano kati ya mataifa hayo mawili ili kugawanya maslahi yao ya ushindi nchini Poland na Ulaya nzima.
Bila hofu ya kuichokonoa USSR, mnamo Septemba 1939 serikali ya Nazi ilishambulia Poland, uvamizi ambao ulisababisha Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Wasovieti, kwa upande wao, waliingia Finland mnamo Novemba mwaka huo huo, ambao ulijulikana kama Vita vya Majira ya baridi.
Katika Mgogoro huu matumizi ya Molotov yalipata umaarufu wake.
Vita vya majira ya baridi na mabomu ya nyumbani
Mapitio ya kitabu "A Frozen Hell: The Russo-Finnish War of the Winter of 1939-1940, na mwanahistoria William Trotter, anatoa maelezo ya kwa nini askari wa Finland waliyaita mabomu yao ya nyumbani kwa jina la "Molotov cocktails".
Mwanadiplomasia Molotov, katika redio ya Sovieti, alisema jeshi la nchi yake wakati wa mgogoro huo halikuwa likiangusha mabomu katika ardhi ya Finland, bali "vifaa na chakula."
Kwa mujibu wake, askari walianza kuita kwa kejeli mabomu ya Soviet "vikapu vya Molotov picnic".
Baadaye, walikubaliana na jina hilo kwa mabomu yao yaliyoboreshwa.
Ingawa makala inahusiana na kuingilia kati kwa USSR nchini Finland, inasema kwamba asili ya mabomu ya Molotov ilianza miaka mingi nyuma, kwa kuwa kuna rekodi za matumizi ya vifaa hivi, kwa mfano, katika Vita vya Wenyewe kwa Wenyewe vya Hispania vya 1936-39.
No comments:
Post a Comment