Tangu Urusi ilipovamia Ukraine, umaarufu wa Rais Volodymyr Zelensky umeongezeka. Baada ya kukabiliana na shambulio la Moscow bila kutarajiwa.
Zelensky anasema ni yeye adui nambari moja wa Urusi , huku familia yake ikiwa ya pili.
Lakini tunafahamu nini kumhusu mke wa rais ambaye hajulikani aliko?
Wenzi hao walifunga ndoa mnamo Septemba 2003, kabla ya kazi ya kisiasa ya Zelensky kuanza. Alisahau sana kumfahamisha mke wake juu ya uamuzi wake wa kugombea urais.Zelenask aligundua kuwa mume wake anagombea urais kwenye mitandao ya kijamii, aliiambia Vogue Ukraine. Alipomuuliza "Mbona hukuniambia?" alijibu: "Nilisahau."
April mwaka 2019, Volodymyr Zelensky alishinda urais wa Ukraine bila kutarajia na kuwa muigizaji na mcheshi asiyekuwa na tajriba ya siasa na uongozi.
Wakati huo ni kundi dogo la watu, hususan watumbuizaji, walimjua mke wake Zelenask at the time.
"Mimi sio mtu mashuhuri napenda kujificha nyuma ya pazia. Mume wangu ni mtu anayejulikana sana na mimi sijui chohote kuhusiana na siasa na ucheshi," aliambia jarida la Vogue wakati huo.
Walivyokutana
Olena mwenye umri wa miaka 44 alizaliwa Kryvyi Rih eneo la kati mwa Ukraine.
Alikutana na Zelensky katika chuo kikuu ambako alikuwa akisomea uanasheria. Inasemekana alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine wakati huo, wakati, Zelensky alikuwa akipambana kujiimarisha kama mcheshi.
Uhusiano wao ulianza wakati Olena alipojiunga kampuni ya Kvartal 95, ambayo ilianzishwa na Zelensky, kuandika hadihi za vichekesho na filamu.
Olena na Volodymyr walikuwa pamoja kwa miaka minane kabla ya kufunga ndoa mwaka 2003 na kuzaa na watoto wawili Sasha na Cyril.
Kampuni hiyo imetayarisha filami inayoitwa "Public Servants" kumuangazia Zelensky kama mwalimu wa shule ambaye ghafla alikuwa rais wa Ukraine. Alichoigiza katika filamu hiyo baadaye ilikuja kuwa kweli kiuhalisia.
Zelenska aliendelea kfanyia kazi Kvartal 95 kabla ya shambulio, lakini alisema alikuwa akitenga muda wa kuhudumia ofisi yar ais na ofisi ya kampuni.
Jukumu lake katika vita
Zelenska mara kwa mara ameandika katika mitandao ya kijamii kuelezea masikitiko yake kuhusu uvamizi wa Urusi dhidi ya nchi yake.
"Watoto wa Ukraine kila mara wanakimbizwa hadi kwenye majengo ya chini ya ardhi ili kuepuka mashambulizi hayo. Hatutaki vita, lakini hatutakata tamaa na tutapinga," aliandika kwenye akaunti yake ya Instagram
Rais Zelensky Zelensky anasema Urusi imeifanya familia yake kuwa mlengwa wake wa pili, mkewe Zelenska na watoto wao wawili, Aleksandra na Kirill.
Hawajaonekana pamoja tangu Siku ya Wapendanao, huku sehemu alipo yeye na watoto ikiwekwa siri kufuatia uvumi kwamba vikosi vya mauaji vinaamiwa kuzunguka mjini Kyiv kumtafuta mume wake.
Licha ya hayo Bi Zelenaska anaunga kikamilifu upinzani unaoongozwa na mume wake nchini Ukraine dhidi ya Urusi. Wiki moja kabla ya uvamizi wa Urusi, Telegram iliandika katika tovuti yake:
"Leo sitashtuka wala kulia machozi,nitatulia na kujiamini, Watoto wangu wananitazama, nasimama na familia yang una watu wote wa nchi yangu."
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA:Urusi yajitayarisha kwa mashambulizi makali zaidi dhidi ya Kyiv huku raia wanaotoroka wakiuawa
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
No comments:
Post a Comment