Waziri Mkuu wa zamani wa Urusi, Mikhail Kasyanov, haamini kwamba Rais Vladimir Putin ametilia uzito kuhusu mazungumzo ya amani, na hakuna uwezekano wa kutoa suluhu la mzozo "ambalo litakuwa starehe kwa watu wa Ukraine".
Zaidi ya ahadi ya kutoegemea upande wowote - ambayo ina maana kwamba Ukraine haitoomba kuwa sehemu ya Nato au EU - Kasyanov anaamini Putin atasisitiza "kutambuliwa rasmi" kwamba Crimea ni sehemu ya Urusi.
"Hilo ni muhimu kabisa, Bw Putin ana wazimu kuhusu Crimea," aliambia BBC World News.
Kasyanov - ambaye alikuwa waziri mkuu kati ya 2000-2004 - alisema ana shaka kuwa makubaliano yoyote yatakwama kutokana na mazungumzo ya sasa kati ya pande hizo mbili, akipendekeza ilikuwa tu kuwapa Warusi "muda wa kujipanga upya".
Alisema Putin na washirika wake wa karibu wa kisiasa walikuwa na "wasiwasi" kuhusu kiwango cha vikwazo "vibaya" vya kiuchumi vilivyowekwa na nchi za Magharibi, akipendekeza kiongozi huyo wa Urusi "hakutarajia vikwazo hivyo vingekuwa vikali."
Lakini alisema uamuzi wowote wa kusitisha operesheni za kijeshi nchini Ukraine "utakuwa mwanzo wa mwisho wa [Putin]".
"Nadhani ataendelea kukandamiza na kuongeza uvamizi," alisema Kasyanov, akiongeza kuwa "alikuwa na wasiwasi sana ... kwamba kitu cha kutisha kinaweza kutokea katika uwanja wa vita".
Unaweza pia kusoma:
YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
No comments:
Post a Comment