Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 19.03.2022: Haaland, Silva, Tuchel, Tielemans, Messi, Tchouameni - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Saturday 19 March 2022

Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 19.03.2022: Haaland, Silva, Tuchel, Tielemans, Messi, Tchouameni

 

m

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Matumaini ya Real Madrid ya kuipiku Manchester City katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 21 kutoka Borussia Dortmund yanazidi kufifia. (Goal)

m

Kiungo wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva, 27, anafikiria kurejea katika klabu ya nyumbani ya Benfica katika miaka miwili ijayo. (Mail)

Meneja wa Chelsea Thomas Tuchel ametupilia mbali tetesi zinazomuhusisha kutaka kuhamia Manchester United, akisema klabu yake ya Stamford Bridge club "inakila kitu kinachotakiwa kunifanya niwe na furaha". (Metro)

Manchester City wanatarajia kumuongezea mkataba kiungo wake wa Hispania Rodri, 25 ambaye mkataba wake wa sasa unakwenda mpaka mwaka 2025. (Telegraph - subscription required) 

mm

Kiungo wa Ubelgiji Youri Tielemans, ambaye ana mkataba na Leicester City unaomalizika mwaka 2023, anasema mazungumzo yanaendelea na Foxes kuhusu mustakabali wake na nyota huyo mwenye miaka 24 atafanya uamuzi mwishoni mwa msimu. (Metro)

m

Mlinzi Mbrazil Dani Alves, 38, anasema mchezaji mwenzake wa Barcelona Lionel Messi hafurahii maisha pale Paris St-Germain na anatumaini mshambuliaji huyo Muargentina mwenye miaka 34 anaweza kurudi Nou Camp. (Mirror)

Klabu za Manchester United na Inter Milan zinamfuatilia mlinzi wa Fiorentina na Serbia Nikola Milenkovic, 24. (Football Italia)

Real Madrid inavutiwa na kiungo wa Monaco Aurelien Tchouameni lakini nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa anafikiria kuelekea ligi kuu England, huku vilabu vya Liverpool, Manchester City na Manchester United vikionyesha kuvutiwa na kinda hilo lenye miaka 22. (Marca)

mm

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Kipa wa Manchester United David de Gea, 31, ametemwa kwenye kikosi cha Hispania kitakachocheza mechi za kirafiki dhidi ya Albania na Iceland kwa sababu haendani na mfumo wa uchezaji wa timu hiyo. (Manchester Evening News)

Manchester City imekubaliana na mpango wa £5.4m kumsajili mshambuliaji wa Atletico Mineiro Savio, 17, ambaye anachezea timu za vijana za Brazil. (Goal)

West Ham imeungana na Newcastle United kumfuatilia kiungo mfaransa Ludovic Blas, 24 ambaye anachezea Nantes. (Football Transfers)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here