Roman Abramovich: Ushahidi mpya wa mikataba ya kifisadi ya bilionea huyu wa Kirusi. - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday 15 March 2022

Roman Abramovich: Ushahidi mpya wa mikataba ya kifisadi ya bilionea huyu wa Kirusi.

 

th

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Uchunguzi wa BBC umebaini kuwepo kwa ushahidi mpya kuhusu mikataba ya ufisadi ambayo ilimtajirisha Roman Abramovich.

Mmiliki huyo wa Chelsea ametengeneza mabilioni ye dola baada ya kuinunua kampuni ya mafuta kutoka kwa serikali ya Urusi katika mnada tata wa mwaka 1995.

Bw. Abramovich alilipa karibu $250m (£190m) kwa Sibneft, kabla ya kuiuza tena kwa serikali ya Urusi kwa $13bn mwaka 2005.

Mawakili wake wanasema hakuna msingi wa kudai kuwa amekusanya utajiri mkubwa sana kupitia uhalifu.

Bilionea huyo wa Urusi aliwekewa vikwazo na serikali ya Uingereza wiki iliyopita kutokana na uhusiano wake na rais wa Urusi Vladimir Putin.

Mali za Abramovich zimezuiliwa na ameondolewa kwenye nafasi ya Ukurugenzi wa klabu ya Chelsea.

Bilionea huyo wa Urusi tayari amekiri katika mahakama ya Uingereza kwamba alifanya malipo ya ufisadi ili kusaidia kufikia makubaliano ya Sibneft.

Mengi zaidi unayoweza kusoma

Alishtakiwa huko London na mshirika wake wa zamani wa biashara Boris Berezovsky mnamo 2012.

Bw Abramovich alishinda kesi hiyo, lakini alieleza mahakamani namna gani mnada wa awali wa Sibneft ulimpa mazingira bora kwake kushinda biashara hiyo na jinsi alivyompa Bw Berezovsky kiasi cha $10m kumlipa afisa wa Kremlin.

BBC Panorama imepata nyaraka inadhaniwa kupaikana kwa njia ya magendo kutoka Urusi.

Nyaraka hiyo ilitolewa kwa njia hiyo na chanzo cha siri, ambaye anasema ilinakiliwa kwa siri kutoka kwa faili za Bw Abramovich na taasisi za kutekeleza sheria za Urusi.

BBC haiwezi kuthibitisha hilo, lakini kupitia vyanzo vingine nchini Urusi umethibitisha maelezo mengi yaliyokuwepo katika waraka huo wa kurasa tano.

Waraka huo unasema kuwa serikali ya Urusi iliibiwa dola $2.7bn za mpango wa Sibneft - madai yaliyoungwa mkono na uchunguzi wa bunge la Urusi wa mwaka 1997. Waraka huo pia unasema kuwa mamlaka za Urusi zilitaka kumshtaki Bw Abramovich kwa udanganyifu.

Inasema: "Wachunguzi wa Uhalifu wa Kiuchumi walifikia hitimisho kwamba ikiwa Abramovich angefikishwa mahakamani angekabiliwa na mashtaka ya udanganyifu... na kikundi cha uhalifu kilichopangwa."

BBC Panorama ilimfuatilia mwendesha mashtaka mkuu wa zamani wa Urusi, ambaye alichunguza makubaliano hayo katika miaka ya 1990.

Yuri Skuratov hakujua kuhusu nyaraka hiyo ya siri, lakini alithibitisha maelezo mengi juu ya uuzaji wa Sibneft.

Bwana Skuratov aliiambia BBC: "Kimsingi, ilikuwa mpango wa udanganyifu, ambapo wale walioshiriki katika ubinafsishaji waliunda kikundi kimoja cha uhalifu ambacho kiliruhusu Abramovich na Berezovsky kuidanganya serikali na sio kulipa pesa za thamani halisi ya kampuni hii."

Nyaraka hiyo pia inaashiria kwamba Bw Abramovich alilindwa na rais wa zamani wa Urusi Boris Yeltsin.

Inasema faili za nyaraka za utekelezaji wa kisheria wa mpango huo juu ya Bw Abramovich zilihamishiwa Kremlin kabla ya uchunguzi uliokuwa unafanywa na Bwana Skuratov kusimamishwa na rais.

Nyaraka hiyo inasema: "Skuratov alikuwa akiandaa kesi ya jinai kwa ajili ya uporaji wa Sibneft kwa misingi ya uchunguzi wa ubinafsishaji wake. Uchunguzi huo ulisimamishwa na rais Yeltsin ... Skuratov alifukuzwa kazi."

Bwana Skuratov alifutwa kazi baada ya kutolewa kwa mkanda wa ngono mwaka 1999. Yeye alihusisha na uchunguzi aliokuwa akifanya akisema ilikuwa ni hatua ya kumdhalilisha yeye na uchunguzi aliokuwa aufanya.

Alisema: "Suala lote lile lilikuwa la kisiasa, kwa sababu katika uchunguzi wangu uligusa kwa ukaribu familia ya Boris Yeltsin, ikiwa ni pamoja na kupitia uchunguzi huu wa ubinafsishaji wa Sibneft."

Bw Abramovich ameendelea kubakia kuwa mtu wa karibu na Ikulu ya Kremlin wakati Vladimir Putin alipoingia madarakani mwaka 2000.

Nyaraka iiyo ina maelezo ya mnada mwingine ulioghushiwa miaka miwili baadaye, ikihusisha kampuni ya mafuta ya Urusi inayoitwa Slavneft.

Bw Abramovich aliunda ushirikiano na kampuni nyingine kununua Slavneft, lakini kampuni hasimu ya China ilikuwa inapanga kununua zabuni karibu mara mbili zaidi ya ofa ya kina Abramovich.

Watu wengi wenye nguvu - kutoka Kremlin hadi bunge la Urusi - waliona ni kama kupoteza ikiwa Wachina wangeshinda zabuni hiyo.

Waraka huo unasema kuwa mjumbe wa ujumbe wa wazabuni hao wa China alitekwa nyara wakati walipowasili Moscow kwa ajili ya mnada huo.

Vladimir Milov alikuwa naibu waziri wa nishati wa Urusi wakai wa zoezi la uuzaji wa Slavneft. Hakuzungumzia kisa hicho cha utekaji nyara, lakini alisema viongozi wa ngazi za juu wa kisiasa tayari waliamua kwamba ushirikiano wa Bw Abramovich utashinda zabuni hiyo.

"Nilisema, angalia, Wachina wanataka kuingia na wanataka kulipa bei kubwa zaidi. Walisema haijalishi, nyama, haikusu. Tayari uamuzi ushafanywa.

Hakuna maoni kwamba Bw Abramovich alijua chochote kuhusu njama ya utekaji nyara, au kushiriki katika hilo.

Mawakili wake wameiambia BBC kuwa madai ya utekaji nyara "hayana ukweli wowote" na "hajui tukio kama hilo".

Pia Mawakili wa Bw Abramovich wanasema madai ya ufisadi katika mikataba ya Slavneft na Sibneft ni ya uongo, na anakanusha kuwa alilindwa na Bwana Yeltsin.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here