Saudi Arabia yawanyonga watu 81 kwa siku moja - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Sunday 13 March 2022

Saudi Arabia yawanyonga watu 81 kwa siku moja


Unyongaji wa hapo awali umesababisha maandamano kama haya huko New York miaka mitatu iliyopita

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Saudi Arabia imesema iliwanyonga watu 81 siku ya Jumamosi - zaidi ya ilivyokuwa mwaka jana wote.

Kundi hilo - ikiwa ni pamoja na Wayemeni saba na raia mmoja wa Syria - walitiwa hatiani kwa "uhalifu mwingi wa kutisha", ikiwa ni pamoja na ugaidi, shirika la habari la serikali SPA lilisema.

Baadhi walishtakiwa kwa kuwa wafuasi wa kundi la Islamic State (IS), al-Qaeda au waasi wa Houthi nchini Yemen.

Mashirika ya haki yanasema kuwa wengi hawapati kesi za haki nchini Saudi Arabia, madai ambayo serikali inayakataa.

Kwa mujibu wa SPA, kundi la hivi punde lilikuwa limehukumiwa na majaji 13 na kupitia mchakato wa kimahakama wa hatua tatu.

Walishutumiwa kwa kupanga mashambulizi dhidi ya malengo muhimu ya kiuchumi, kuua au kulenga askari wa vikosi vya usalama, utekaji nyara, utesaji, ubakaji na kuingiza silaha nchini humo.

Saudi Arabia ina moja ya viwango vya juu zaidi vya wanaonyongwa duniani - ya tano katika orodha ya Amnesty International, nyingine nne zikiwa ni China, Iran, Misri na Iraq.

Iliwanyonga watu 69 mwaka jana.

Nchi tatu zenye idadi ya juu ya watu walionyongwa;

IRAN

Moja ya mataifa yanayotekeleza zaidi adhabu ya kifo ulimwenguni. Takwimu rasmi kutoka Shirika la takwimu la masuala ya adhabu za vifo (DPIC), inaonyesha kuwa nchi hiyo imenyongwa watu zaidi ya 3,700 katika kipindi cha miaka tisa kati ya 2011 mpaka 2021.

Mwaka 2019 pekee zaidi ya watu watu 251 walinyogwa kwa makosa mbalimbali, ikiwa ni pungufu kwa watu watatu ukilinganisha na mwaka 2018. Lakini mwaka 2015 ilifikia idadi kubwa zaidi ya kunyonga watu 977.

MISRI

Nchi ya Misri inatajwa kuongoza Afrika, ikiwa miongoni mwa nchi tano za juu duniani zinazotekeleza adhabu ya kifo kwa kiwango cha juu.

Kwa mfano katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013 mpaka 2020, idadi ya watu walionyongwa nchini Misri inakadiriwa kuvika 150, ambayo ni mara kenda zaidi ya ile ya mwaka 2013 walipongonywa watu 32 tu.

Ingawa katika kipidi cha miaka miwili kati ya 2018 na 2019 Misri ilitoa hukumu ya kifo kwa watuhumiwa1,152 wa makosa mbalimbali lakini iliwanyonga watu 75 pekee. Huku wengine maelfu wakisubiri kutekelezwa kwa adhabu hiyo.

IRAQ

Kati ya mwaka 2011 mpaka 2019 Iraq imenyonga watu zaidi ya 800, wakati mwaka 2020 pekee chi hiyo imenyonga watu 45, ingawa ni pungufu ukilinganisha na mwaka 2019 iliponyonga watu karibu 100, bado idadi hiyo inatajwa kuwa kubwa zaidi unapozungumzia nchi zinazonyonga watu wengi. Kama ilivyo kwa Saudi Arabia, kunyogwa kwa kamba na kwa risasi ni njia inazotumia zaidi. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here