SIMBA YAPANIA KUFANYA VIZURI KIMATAIFA - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 14 March 2022

SIMBA YAPANIA KUFANYA VIZURI KIMATAIFA

 

SALIM Abdallah,’Try Again’ Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba kuwa malengo ya timu hiyo kimataifa ni kuweza kufanya vizuri kwenye mechi ambazo watacheza.

Kwenye kundi D la Kombe la Shirikisho Simba ni namba moja ikiwa na pointi 7 baada ya kucheza mechi 4 inafuatiwa na ASEC Mimosas iliyo nafasi ya pili na pointi 6 kibindoni.

Ushindi ambao waliupata Machi 13, Uwanja wa Mkapa mbele ya RS Berkane uliwafanya waweze kutoboa mpaka kufika hapo walipo kwa bao la kiungo Pape Sakho ilikuwa dakika ya 44 kwa pasi ya Meddie Kagere.

Try Again amesema:”Malengo yetu ni kuweza kufanya vizuri kwenye mechi zetu ambazo tunacheza kimataifa na lengo ni kuona tunapata matokeo mazuri.

“Ushindani ni mkubwa hilo tunalijua lakini uzoefu ambao tunao kwenye mashindano ya kimataifa unatufanya tuamini kwamba tunaweza kazi bado inaendelea na sio kitu chepesi.

“Kikubwa ni kuona kwamba mashabiki wanazidi kuwa nasi ili tuweze kufanya vizuri zaidi na zaidi,” amesema.

Mchezo ujao wa Simba kimataifa ni dhidi ya ASEC unatarajiwa kuchezwa Jumapili ya Machi 20 itakuwa ugenini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here