TANZANIA COMMERCIAL BANK YAZINDUA KADI YA MALIPO YA KIMATAIFA YA POPOTE VISA CARD - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday 23 March 2022

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAZINDUA KADI YA MALIPO YA KIMATAIFA YA POPOTE VISA CARD

 



Makamu wa Rais wa VISA card Africa Mashariki Corine Nana (kulia), na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi wakiminya kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Popote Visa Card iliyozinduliwa na Tanzania Commercial Benki kwaajili ya kuwarahisishia wateja wa Benki hiyo kupata huduma yoyote na wakiwa sehemu yoyote ndani na nje ya nchi hafla ya uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam




Makamu wa Rais wa VISA card Africa Mashariki Corine Nana (katikati) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Sabasaba Moshingi wa pili kushoto wakionesha mfano wa POPOTE VISA CARD wakati wa uzinduzi rasmi wa kadi hiyo iliyozinduliwa na Tanzania Commercial Bank wengine pichani ni pamoja na Mkurugenzi wa Teknohama wa Tanzania Commercial Bank Jema Mssuya, Mkurugenzi Mtendaji wa UBX Tanzania LTD, Seronga pamoja na Meneja Mwandamizi wa Intanet Banking wa TCB Allen Manzi hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.



Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Popote Visa Card iliyozinduliwa na Tanzania Commercial Benki kwaajili ya kuwarahisishia wateja wa Benki hiyo kupata huduma yoyote na wakiwa sehemu yoyote ndani na nje ya nchi hafla ya uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam



Makamu wa Rais wa VISA card Africa Mashariki Corine Nana (kulia), akikabidhi kadi ya POPOTE VISA CARD kwa mmoja ya wateja waliohudhulia uzinduzi rasmi wa Popote Visa Card iliyozinduliwa na Tanzania Commercial Benki kwaajili ya kuwarahisishia wateja wa Benki hiyo kupata huduma yoyote na wakiwa sehemu yoyote ndani na nje ya nchi hafla ya uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam (katikati) ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi.



Mteja wa Tanzania Commercial Bank akionesha kadi ya POPOTE VISA CARD iliyozinduliwa leo na Benki hiyo bara baada ya kukabidhiwa.




picha ya Pamoja




Benki ya Biashara Tanzania (TCB) jana imezindua kadi ya malipo ya kidijitali ambayo itaisaidia Serikali ya Awamu ya Sita kufanikisha mpango mkakati wake wa kuifanya Tanzania kuwa uchumi usiotegemea sana fedha taslimu.

Huduma hiyo ya malipo ya kimataifa inayojulikana kama Kadi ya Popote Visa ni matokea ya ushirikiano kati ya TCB na Visa International ya Marekani inayoongoza duniani katika teknolojia bunifu za malipo ya kidijitali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wake jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bw Sabasaba Moshingi alisema Popote Visa Card ina uwezo wa hali ya juu kusaidia kutimiza ndoto za taasisi hiyo ya kuendeleza huduma jumuisha za kifedha nchini.

TCB na mshirika wake wameazimia kuunga mkono juhudi za kitaifa za kujenda uchumi wenye matumizi madogo ya fedha taslimu kwa kuwekeza katika suluhisho bunifu za malipo ya kidijitali ambazo ni rahisi zaidi, salama na zinazozingatia ufanisi wa usimamizi wa fedha.

“Huduma kama kadi ya malipo ya kimataifa tuliyozindua leo na ushirikiano wetu na kampuni ya Visa ni muhimu sana katika juhudi za serikali kujenga uchumi wa kidijitali na kuifanya Tanzania kuwa taifa lisilotegemea sana malipo yanayofanywa kwa fedha taslimu,” Bw Moshingi alibainisha.

Aliwaambia waandishi wa habari kuwa uamuzi wa TCB kushirikiana na Visa unatokana na kampuni hiyo kuwa kigogo wa teknolojia za malipo duniani ikiwa na mtandao wa wafanyabiashara milioni 61 wa kimataifa.

Wakizungumza wakati wa uzindunzi huo, maafisa waandamizi wa Visa Afrika Mashariki, walisema dhamira ya kampuzi hiyo si tu kuongeza matumizi ya kadi za kidijitali nchini peke yake bali duniani kote kuwahudumia wananchi, wafanyabiashara na serikali mbalimbali.

Makamu wa Rais wa Visa na Mkurugenzi Mtendaji wake wa Afrika Mashariki, Bi Corine Mbiaketcha Nana, alisema Tanzania ina kila kitu kinachohitajika kuwa uchumi wa kisasa zaidi wa kidijitali.


“Kama suluhisho zote bunifu za malipo ya kidijitali, matumizi ya Popote Visa Card yana manufaa mengi na faida kubwa kwa watu binafsi, mashirika na serikali,” Bi Nana alifafanua na kusisitiza kuwa mchango wake mkubwa hasa kwa wananchi wa kawaida ni maendeleo ya huduma jumuishi za kifedha.

Uzinduzi wa UCB Popote Visa Card umefanyika wiki mbili bada ya serikali kutangaza mipango na uwekezaji wake kwenye ujenzi wa uchumi usiotegemea sana fedha taslimu kupitia Mpango wa Tanzania ya Kidijitali.

Kwa mujibu wa Waziri wa TEHAMA, Bw Nape Mnauye, hivi karibuni Tanzania ilipata mkpo nafuu kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya utekelezaji wa azma hiyo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 150.

Wakizumgumza kwa nyakati tofauti twakati wa uzunduzi wa bidhaa hiyo mpya sokoni wateja na wandau mbalimbali wa TCB walisema kuzinduliwa kwa kadi hiyo mpya kutasaidai michakato mbalimbali ya kuharakisha maendfeleo ya kidijitali nchini.

“Ushirikiano wa kimkakati kati ya TCB na Visa si tu unazinufaisha taasisi hizo mbili peke yake, bali pia utasaidia kupanua wigo wa malipo ya kidijitali nchini na kuongeza faida za kibiashara katika nyororo wa thamani wa malipo kitaifa,” Meneja Mkuu wa dt card Tanzania, Bw Christiaan Wielengs, alibainisha.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here