Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 09.03.2022: Rudiger, Gnabry, Adeyemi, Mahrez, Milinkovic-Savic, Calvert-Lewin - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday 9 March 2022

Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 09.03.2022: Rudiger, Gnabry, Adeyemi, Mahrez, Milinkovic-Savic, Calvert-Lewin

 

Thomas Tuchel and Antonio Rudiger

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel na mchezaji Antonio Rudiger

Newcastle United wanataka kumsajili mlinzi wa Ujerumani Antonio Rudiger wakati mkataba wa kiungo huyo wa Chelsea wa miaka 29-utakapomalizika mwisho wa msimu huu. (Telegraph)

Lakini Manchester United watamenyana na watesi wao wa Ligi ya Primia kumpata Rudiger msimu huu wa joto. (Express)

United, hata hivyo huenda wakakosa nafasi ya kumsaini beki huyo kutokana na sintofahamu y ani nani atakuwa kocha uwanjani Old Trafford. (90min)

Arsenal huenda wakajaribu kumsajili tena winga wa Ujerumani Serge Gnabry kutoka Bayern Munich, huku thamani ya kiungo huyo wa miaka 26 - aliyekuwa na Gunners kwa miaka minne - ikikadiriwa kuwa £63m. (Football.London)

Serge Gnabry

CHANZO CHA PICHA,EPA

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund wa miaka 21- Mnorway Erling Braut Haaland anataka kujiunga na Barcelona msimu huu wa joto. (Sport - in Spanish)

Hata hivyo, rais wa Barcelona Joan Laporta amekanusha madai kwamba mashauriano ya kumsajili Haaland ambaye pia anatakiwa na Manchester City na Real Madrid tayari yanaendelea. (Mail)

Mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 28, amewaambia wachezaji wenzake kwamba atasalia Tottenham msimu ujao ikiwa watafuzu kwa soka ya Ligi ya Mabingwa na Antonio Conte atabaki kama kocha. (Express)

Match-winner Harry Kane celebrates Spurs' victory

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane

Tottenham wanajiandaa kupokea maombi ya kumununua mlinzi wa miaka 23- Mbrazil Emerson Royal, chini ya mwaka mmoja baada ya kumnunua kwa £26m kutoka Barcelona. (Sun)

Liverpool watapata fursa ya kumsajilimshambuliaji wa Red Bull Salzburg wa miaka 20- Mjerumani Karim Adeyemi msimu wa joto dirisha la uhamisho litakapofunguliwa, hata hivyo, huenda wakakabiliwa na ushindani kutoka kwa Borussia Dortmund. (Express)

Paris St-Germain na Chelsea wanataka kumsaini wingi wa Manchester City na Algeria Riyad Mahrez, 31. (Foot Mercato)

Bernardo Silva na Riyad Mahrez (right)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Bernardo Silva(kushoto) na Riyad Mahrez (kulia) wakishangilia bao la Manchester City

RB Leipzig wamejiunga na mbio za kumsaka mlinzi wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 19 Mhispania Rafa Marin. (Marca - in Spanish)

Manchester United watalazimika kulipa hadi euro milioni 80 (£66m) kumsajili kiungo wa kati wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 27, kutokana Lazio kuchukua nafasi ya kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 28. (Sport Witness)

Winga wa zamani wa Arsenal Perry Groves anasema Gunners wanatakiwa kumlenga mshambulizi wa Everton na Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 24, mwisho wa msimu. (Star)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here