Tetetsi za soka Ulaya Alhamisi 03.03.2022: Ancelotti, Mbappe, Rodriguez, McGregor, Johnson - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 2 March 2022

Tetetsi za soka Ulaya Alhamisi 03.03.2022: Ancelotti, Mbappe, Rodriguez, McGregor, Johnson

 

Carlo Ancelotti miongoni mwa mameneja wanaotaka kuifunza Man United

CHANZO CHA PICHA,EPA

Maelezo ya picha,

Carlo Ancelotti miongoni mwa mameneja wanaotaka kuifunza Man United

Meneja wa Real Madrid Muitaliano Carlo Ancelotti, 62, ameibuka kuwa mgombea wa kushangaza anayewania kuwa meneja mpya ajaye wa Manchester United. (Times - subscription required)

Kiungo wa Colombia aliyewahi kuichezea Everton James Rodriguez, 30, ameiweka mguu sawa "the Toffees" baada ya kugusia uwezekana wa kurejea kwenye klabu hiyo akitokea Qatar. (Express)

Paris Saint-Germain wanajiandaa kumpa mkataba mpya mshambuliaji wake Kylian Mbappe,23 wenye thamani ya £799,000 kwa wiki ili kusalia klabuni hapo, huku Real Madrid wakimuwania pia mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa. (Le Parisian, via Star)

Kylian Mbappe

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kylian Mbappe

Bayern Munich, Tottenham na Arsenal zinamuwania mlinzi wa kulia wa Middlesbrough muingereza Djed Spence, 21, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Nottingham Forest. (Sky Sports)Hata hivyo vilabu vyote vya Tottenham na Arsenal, pamoja na Liverpool, pia vinafikiria kupeleka dau kwa ajili ya kumnasa mlinzi wa kulia wa Torino, raia wa Ivory Coast Wilfried Singo, 21, ambaye atapatikana kwa kitita cha £15m. (Football London)

Barcelona wana matumaini ya kumshawishi mlinzi wa Chelsea na Denmark Andreas Christensen, 25, na mchezaji mwenzake Cesar Azpilicueta, 32 raia wa Hispania kujiunga na klabu hiyo kwa uhamisho huru mwishoni mwa msimu. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Andreas Christensen

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Andreas Christensen

Meneja wa Nottingham Forest Steve Cooper anasema kiungo mshambuliaji wa Wales Brennan Johnson, 20, atavurugwa na mazungumzo ya mkataba mpya au nia za kutakwa na vilabu vya ligi kuu England. (Mirror)

Nyota wa UFC kutoka Ireland Conor McGregor, 33, ameonyesha nia yake ya kutaka kuinunua Chelsea baada ya mmiliki wake Roman Abramovich kusema ana mpango wa kuiuza klabu hiyo. (Twitter)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here