Ukraine na Urusi: Makubaliano ya kumaliza vita Ukraine yako karibu kiasi gani? - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday 22 March 2022

Ukraine na Urusi: Makubaliano ya kumaliza vita Ukraine yako karibu kiasi gani?

 

Vladimir Zelensky na Vladimir Putin huko Paris, picha ya kumbukumbu. Mnamo 2019, mikutano kama hiyo bado iliwezekana

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mazungumzo ya upatanishi ya wajumbe wa Urusi na Ukraine Jumatatu, Machi 21, yalidumu kwa saa moja na nusu, baada ya hapo majadiliano yaliendelea katika muundo wa kujigawa kwenye makundi, alisema mjumbe wa Ukraine, na kiongozi wa wabunge wa cha chama tawala cha Ukraine "Servant of the People" David Arahamiya.

Je mazungumzo haya yamefikia wapi? kuna maendeleo yoyote yanayoonekana? na ni aina gani ya makubaliano yanayotafutwa kutoka kwa kila upande? Urusi inayoshambulia na Ukraine inaojitetea?

Kuhitimisha kupitia kauli za vyama inaweza ikwawa sio rahisi, kwani wakati mwingine huonekana kama ni taarifa tu kivita. BBC inajaribu kueleza kwa kifupi kile kinachofahamika mpaka sasa kuhusu mwenendo wa mazungumzo kati ya Ukraine na Urusi.

Mwanzo wa Mazungumzo

Mazungumzo yalianza Februari 28, ilikuwa siku ya tano ya uvamizi wa majeshi ya Urusi nchini Ukraine, wakati wawakilishi wa pande hizo mbili zinazozozana walikutana kwa mara ya kwanza huko Belarus, katika mkoa wa Gomel, kwenye mpaka wa Ukraine karibu na Mto Pripyat.Ujumbe wa Urusi uliongozwa na mmoja wa wasaidizi wa karibu wa Rais Vladimir Putin, Vladimir Medinsky, Waziri wa zamani wa Utamaduni na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Historia ya Kijeshi ya Urusi. Upande wa Ukraine uliongozwa na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Oleksiy Reznikov na mshauri mkuu wa ofisi ya rais Mykhailo Podolyak.

Awamu ya kwanza ya mazungumzo haikuzaa matunda yoyote. Na ilipofika Machi 1, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema yuko tayari kuzungumza moja moja na Vladimir Putin. Lakini hakukuwa na hatua kubwa iliyopigwa.

Mikhail Podolyak anaongoza ujumbe wa Ukraine

CHANZO CHA PICHA,ANADOLU AGENCY VIA GETTY IMAGES)

Mnamo Machi 7, duru ya tatu ya mazungumzo ilifanyika huko Belovezhskaya Pushcha, ambayo pande zote mbili zilizungumza: mkuu wa ujumbe wa Urusi Medinsky alisema kuwa matarajio yao hayakufikiwa, na mkuu wa ujumbe wa Ukraine, Mykhailo Podolyak, akaripoti mazungumzo hayo yalikuwa na maendeleo madogo tu.

Machi 10, Uturuki ilijaribu kuwaleta pamoja mawaziri wa mambo a kigeni wa Urusi na Ukraine, Sergey Lavrov na Dmitry Kuleba, akihudhuria pia waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut huko Antalya. Baada a kikao hicho, Kuleba alisema hakuna hatua iliyopigwa hasa kwenye kusitisha mapigano.

Muktadha mpya wa mazungumzo

Siku ya Jumatatu, Machi 21, Ukraine na Urusi zilibadilishana tena taarifa juu ya mazungumzo ya ngazi ya juu. Rais Zelensky amesema fursa pekee ya Rais Putin ya kuepuka maafa kwa Urusi ni kufanya mazungumzo ya amani.

Msemaji wa Kremlin Peskov aliweka wazi kwamba ni mapema mno kuzungumzia uwezekano wa mkutano kati ya Vladimir Putin na Vladimir Zelensky, kwa sababu "hawatakuwa na chochote cha kurekebisha, bado hakuna makubaliano."

Tangu kuanza kwa vita na tangu mwanzo wa mazungumzo ya kwanza, mambo mengi yamebadilika - kwa pande zote kwa Ukraine na kwa Urusi. Mashambulizi ya mara kwa mara ya makombora na silaha yaliyofanywa na wanajeshi wa Urusi - ikiwa ni pamoja na kuwalenga raia - yalisababisha kuwepo kwa mamilioni kadhaa ya wakimbizi, raia wengi kujeruhiwa na uwepo wa janga la kibinadamu katika mikoa kadhaa ya Ukraine.

Vladimir Putin anafanya kila kitu kuonyesha kwamba vikwazo vya Magharibi sio vya kutisha

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Hata hivyo, wachambuzi wa Magharibi wanakubaliana kwamba mambo hayaendi kwa kulingana na mpango wa Kremlin, ambao vikosi vyake vimefungwa katika vita dhidi ya majeshi ya Ukraine, ambayo yanapambana kupinga uchokozi wao.

Jinsi mazungumzo yanavyoendelea

Licha ya ukweli kwamba mchakato wa mazungumzo, kulingana na wawakilishi wa Ukraine, ni "magumu", na kwa taarifa za kuvuja mara kwa mara za mazungumzo kutoka pande zote mbili kuna taarifa za matumaini - kwamba kuna fursa ya kufikia maelewano na baadhi ya mambo muhimu ya mkataba wa baadaye yanakaribia kukubaliwa.

Volodymyr Zelenskyy katika moja ya mikutano ya waandishi wa habari alisema kuwa mazungumzo yalijaa maudhui kwamba: Wawakilishi wa Ukraine na Urusi wanajadili masuala fulani, walianza kuzungumza juu ya kitu fulani, na sio kutupa mahitaji ya ukomo."

Vladimir Putin, akimpokea Alexander Lukashenko huko Ikulu ya Kremlin, alisema kuwa mazungumzo hayo "sasa yanafanyika karibu kila siku," "kuna mabadiliko fulani mazuri," alisema bila kueleza kwa kina, alimaanisha nini.

Pande mbili hizi zinataka nini?

Urusi inataka Ukraine kukubali kwamba inapaswa kutoegemea upande wowote na haipaswi kuomba kujiunga na Nato. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky tayari amekubali hilo.

Madai mengine ni kwamba Ukraine italazimika kupitia mchakato wa kuondoa silaha (mipakani) ili kuhakikisha kuwa si tishio kwa Urusi. Lazima kulindwa kwa lugha ya Kirusi nchini Ukraine. Na kuna kitu kinachoitwa de-Nazification.

Mshauri na msemaji mkuu wa Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, Ibrahim Kalin akirejea mazungumzo yaliyosimamiwa na nchi yake alisema kwamba madai mengine ya Urusi yanahusisha hali ya Donbas, mashariki mwa Ukraine, sehemu ambazo tayari zimejitenga na Ukraine na kusisitiza ni sehemu ya Urusi, na hali ya Crimea.

Ingawa Bwana Kalin hakufafanua kwa undani zaidi, ila maelezo yake yanaleta dhana kwamba Urusi itaitaka serikali ya Ukraine kuachia eneo mashariki mwa Ukraine. Hatua hiyo itakuwa ya utata sana.

Volodymyr Zelensky alihutubia Bunge la Israeli, akilinganisha kile kinachotokea Ukraine na mauaji ya Holocaust.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Ukraine yenyewe inataka kuwa huru, ijiamulie inavyotaka ikiwemo uwezekano wa kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Mnamo Machi 16, msemaji wa Vladimir Putin Dmitry Peskov alithibitisha kuwa mazungumzo ya kusitisha mapigano kati ya Urusi na Ukraine yaligusia kuhusu kuwa na Ukraine isiyoegemea upande wowote.

Je Amani inaweza kupatikana hivi karibuni?

Siku ya Jumapili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu alisema kuwa "Ingawa sio rahisi kufikia makubaliano katika vita ambapo raia wanakufa, tungependa kutambua kwamba kasi [ya kutafuta mkataba wa amani] inazidi kuongezeka. Tunaona pande hizi mbili ziko karibu na makubaliano."

Mevlut Cavusoglu yuko kwenye mazungumzo ya kina na Sergey Lavrov

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg katika mahojiano na NBC, ingawa aliishukuru Uturuki kwa juhudi zake za kuunga mkono mazungumzo ya Ukraine na Urusi, lakini alibainisha: "Ni mapema mno kusema kama mazungumzo haya yataleta matokeo yoyote thabiti."

Rais wa Uturuki Volodymyr Zelenskyy katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Marekani CNN siku ya Jumapili alisema: "Nadhani tunahitaji kutumia njia yoyote, nafasi yoyote, ili kuwe na fursa ya mazungumzo, fursa ya kuzungumza na Putin. Lakini ikiwa majaribio haya yatashindwa, itamaanisha mwanzo wa Vita Kuu ya Tatu ya Dunia."

Mengi zaidi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here