Kura rasmi za maoni zilizofanywa na wanasosholojia huru zinaonyesha kwamba Warusi wengi wanaunga mkono vita vya Ukraine. Je, tunaweza kuamini tafiti zao kwa kiasi gani?
70% ya Warusi wanaunga mkono "oparesheni maalum ya kijeshi" nchini Ukraine. 21% wanapinga hatua hiyo na 8% hawajui. Hayo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kituo cha Utafiti wa Maoni ya Umma cha Urusi VSIOM mnamo Machi 5, Asilimia 70 kati ya walioulizwa walisema wanaamini operesheni hiyo inakwenda vyema kwa jeshi la Urusi.
Hazina ya Maoni ya Umma FOM (ambayo hufanya tafiti zilizoidhinishwa na utawala wa rais) inatoa picha sawa. Matokeo yao yanaonyesha 65% ya Warusi wameidhinisha operesheni ya kijeshi nchini Ukraine, 17% wanapinga na 18% hawajui.
Utafiti huru wa mwanaharakati wa upinzani nchini Urusi Alexei Minyailo unaosema "Warusi Hawataki Vita?" pia ulionyesha mseto wa matokeo ya wale wanaopinga vita. 51% ya walioulizwa walisema "Ndiyo", wakati 27% tu ndio walisema "Hapana".Hitimisho moja kutoka kwa uchunguzi huo ni kwamba wengi wa wale wanaounga mkono vita hivyo wanaamini vyombo vya habari vinavyoendeshwa na serikali kwa asilimia (73%), wakati 85% ya wale wanaopinga vita hawafanyi hivyo.
Baadhi ya wale wanaopinga uvamizi wa Ukraine ni vijana waliyo na umri wa chini ya miaka 30. Bado wanastahiki kuitwa au wamemaliza huduma yao ya kijeshi hivi majuzi.
Asilimia ya Warusi wanaopinga vita nchini Ukraine
Utafiti wa mitandao ya kijamii ulitoa picha tofauti na tafiti zilizofanywa kwa njia ya simu.
Takriban 52% ya machapisho kwenye mitandao ya Urusi yanaunga mkono vita wakati 30% yanapinga vita. Bila kujali ikiwa wanaunga mkono au kupinga-, 30% ya Warusi walielezea kusikitishwa na hali wanayopitia Waukraine. Utafiti unasema ni mhemko wa kawaida unaopatikana katika machapisho yote.
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Udhibiti kwa vitendo
Televisheni na tovuti za Ukraine zimesheheni picha za kutisha za vita: nyumba zilizolipuliwa kwa mabomu, raia waliouawa na wengine kujeruhiwa, vifaa vya jeshi la Urusi vilivyoharibiwa au kuchomwa moto. Makumi ya video za wanajeshi na maafisa wa Urusi waliotekwa, damu na maiti zimejaa kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Ukraine.
Lakini ukitazama Televisheni ya Kirusi hutaona ripoti juu ya kushindwa na hasara ya jeshi la Kirusi.
Wiki moja baada ya wanajeshi wa Urusi kuingia nchini Ukraine, serikali ilipitisha sheria ya kuwaadhibu watakaosambaza ripoti ambazo hazijahakikiwa kuhusu jeshi la Urusi. Uwasilishaji wa ripoti zozote ambazo sio za kuaminika kulingana na serikali sasa ni adhabu ya kifungo cha miaka 15 jela.
Vyombo vya habari vya Urusi vimezuiliwa kuita uvamizi wa Ukraine kuwa ni vita na kuagizwa vitumie neno "operesheni maalum".
Vituo ambavyo havikutekeleza agizo hilo vimefungwa. Karibu vyombo vyote huru vya habari vilifungiwa wiki ya kwanza ya vita.
Kabla ya mzozo kuanza, karibu kila chombo cha habari cha Urusi ambacho kilipinga Kremlin na kutoa maoni huru kiliitwa "wakala wa kigeni".
Alexei Bessudnov Mwanasosholojia katika Chuo Kikuu cha Exeter, anasema unapaswa kuangalia kwa makini maneno.
"Asilimia inayounga mkono na asilimia inayopinga inategemea sana jinsi unavyouliza swali.
Unaunga mkono nini? Kila mtu aliuliza swali kwa njia tofauti.
VCIOM iliuliza, Je unaunga mkono uamuzi wa Urusi kuendesha oparesheni maalum nchini Ukraine ?
Inaonekana kuwa swali wastani kwa sababu ulkiuliza, "Unaunga mkoo uamuzi huo" unapata jibu tofauti ikiwa utauliza, "Unafikiria nini kuhusu oparesheni maalum ya kijeshi?"
Kwa hivyo ukiuliza kuhusu oparesheni maalum, hilo ni swali moja. Lakini ukiuliza kuhusu uvamizi wa Ukraine au vita nchini Ukraine, hilo ni swali tofauti kabisa.
Kikubwa kinategemea jinsi unavyouliza swali.
Mbali na hilo, tafakari kupigiwa simu na mtu usiyemjua na kuulizwa maoni yako kuhusu hatua za kijeshi nchini Ukraine. Bila shakawatu watakuwa waangalifu kuhusu kutoa jibu la uwazi.
Na wengi hawajaamua wanafikiri nini haswa. Watatoa maoni yao wakati wa mahojiano, wakiongozwa na mhojiwaji, kulingana na jinsi anavyozungumza, wapi wanaongoza mazungumzo. Maoni ya mtu yanaweza kupingana, yale anayounga mkono, yale ambayo hayatendi.
Tunachoweza kusema kwa hakika kuhusu tafiti hizi ni kwamba 50 - 70% ya Warusi wana uwezekano mkubwa wa kuunga mkono maamuzi ya serikali. Ni kweli? Naam bila shaka, Lakini ikiwa 50-70% inawaunga mkono, basi 30-50% wanapinga au angalau hawajui.
Pia kuna tofauti kubwa kati ya makundi ya kijamii na kiuchumi na tofauti kubwa zaidi ni kati ya makundi ya umri. Watu wengi walio chini ya miaka 30 nchini Urusi hawaungi mkono operesheni maalum ya kijeshi. Na hii inaonekana hasa katika miji mikubwa, hasa St Petersburg. Wakati watu tisa kati ya 10 walio karibu na umri wa kustaafu wataiunga mkono.
Zaidi inategemea unapata wapi taarifa zako. Warusi wengi wazee hupata habari zao kutoka kwa TV. Wanaitazama kila siku na kusikia simulizi mara kwa mara juu ya kupigana na Wanazi na propaganda zingine zote ambazo serikali inaendesha ndani ya saa 24kila siku.
Vijana sio sana kutazama televisheni na muda mwingi wanatumia mitandao, kwa hivyo mazingira yao ya kupata habari ni tofauti kabisa.
Pia kuna tofautikati ya wanaume na wanawake. Hasa wanawake wa umri wa makamo ni wachache wanaunga mkono vita. Kuna tofauti, ingawa sio kubwa sana, kati ya watu waliosoma chuo kikuu na wale ambao hawakusoma. Hasa katika miji, wale waliosoma hawana mwelekeo wa kuunga mkono uvamizi.
Kwa hivyo hakuna makubaliano ya jumla, lakini kuna wachache muhimu. Cha msingi kinategemea sana kile unachouliza na takwimu hii inatarajiwa kutabadilika.
No comments:
Post a Comment