Vita vya Ukraine: Mgogoro unafungua 'mahangaiko duniani' kuhusu bei ya chakula - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday 8 March 2022

Vita vya Ukraine: Mgogoro unafungua 'mahangaiko duniani' kuhusu bei ya chakula

 


th

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, David Beasley, ameonya kwamba mzozo wa Ukraine unaweza kusababisha bei ya chakula duniani kupanda, na kuathiri vibaya watu maskini zaidi duniani.

Ukraine na Urusi zote ni wauzaji wakuu wa vyakula vya kimsingi, na vita tayari vimeathiri uzalishaji wa mazao, na kusababisha bei kupanda.

Bw Beasley alisema inawaweka watu zaidi katika hatari ya njaa duniani kote."Wakati tu unapofikiria jahanamu duniani haiwezi kuwa mbaya zaidi, inakuwa mbaya," alisema.

Urusi na Ukraine, ambazo wakati fulani ziliitwa "kikapu cha mkate cha Ulaya", zinauza nje takriban robo ya ngano ya dunia na nusu ya bidhaa zake za alizeti, kama vile mbegu na mafuta. Ukraine pia inauza mahindi mengi duniani.

line

Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi

line

Wachambuzi wameonya kuwa vita vinaweza kuathiri uzalishaji wa nafaka na hata bei ya ngano maradufu duniani.

Bw Beasley aliambia kipindi cha Business Daily cha BBC World Service kwamba idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani kote tayari imeongezeka kutoka milioni 80 hadi milioni 276 katika miaka minne kabla ya uvamizi wa Urusi, kutokana na kile anachokiita "dhoruba kamili" ya migogoro, mabadiliko ya hali ya hewa na coronavirus.

Alisema baadhi ya nchi zinaweza kuathiriwa haswa na mzozo wa sasa, kutokana na idadi kubwa ya nafaka wanazoagiza kwa sasa kutoka eneo la Bahari Nyeusi.

th

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

"Nchi ya Lebanon, hutoa asilimia 50% ya nafaka zao kutoka Ukraine. Yemen, Syria, Tunisia - na ninaweza kuendelea na kuendelea - zinategemea nchi ya Ukraine kama kikapu cha chakula," alisema.

"Kwa hivyo unaenda kutoka kuwa kikapu cha mkate hadi sasa, kihalisi, kuwapa mkate. Ni kinyume cha ajabu cha uhalisia."

"Kulinda ardhi yetu"

Yara International, ambayo inahudumu katika zaidi ya nchi 60, iliambia BBC kwamba uhaba unaweza kuathiri vibaya mavuno ya mazao, na kusababisha "shida ya chakula duniani".

Mwanasheria wa Ukraine Ivanna Dorichenko, mtaalam wa usuluhishi wa biashara ya kimataifa, alisema baadhi ya wakulima nchini Ukraine tayari wametelekeza mashamba yao ili kuchukua silaha dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Aliambia BBC: "Wanaume wanaohitaji kufanya kazi katika ardhi hiyo, wote wanatetea ardhi yetu hivi sasa. Kwa sababu ikiwa hawatatetea ardhi hiyo, hakutakuwa na kitu cha kufanyia kazi baadaye, na hakuna mtu mmoja hivi sasa ambaye hajaribu kusaidia kwa njia yoyote anayoweza."

Bi Dorichenko alisema vita hivyo vimesababisha uharibifu mkubwa kwa njia za usambazaji bidhaa ambazo kawaida hutumika kusafirisha mazao ya kilimo. Jeshi la Ukraine lilisimamisha meli zote za kibiashara katika bandari zake baada ya uvamizi wa Urusi.

"Meli haziwezi kuondoka majini, meli haziwezi kubeba. Kwa hakika ni eneo la vita. Cha kusikitisha ni kwamba, hakuna kitu ambacho kinaweza kusafirishwa hivi sasa kutoka Ukraine."

Alisema ilimaanisha "hasara kubwa" kwa biashara, lakini pia juhudi za kibinadamu, kwa sababu Ukraine haiwezi tena kutuma bidhaa katika kanda kama vile Kusini Mashariki mwa Asia, Mashariki ya Kati na Afrika, na pia kwa mashirika yasio ya kiserikali kama vile Mpango wa Chakula Duniani.

Huku mfumuko wa bei za vyakula ukiwa tayari katika hatua ya msukosuko katika baadhi ya nchi kabla ya kuzuka kwa uhasama nchini Ukraine, mwanauchumi wa Afrika Kusini Wandile Sihlobo alisema ana wasiwasi kuhusu madhara yanayoweza kutokea kwa mataifa yanayoagiza nafaka barani Afrika na kwingineko.

Bw Sihlobo, mchumi mkuu katika Chemba ya Biashara ya Kilimo ya Afrika Kusini, aliambia BBC kwamba ingawa kupanda kwa bei kunaweza kuwa tatizo katika muda mfupi, uhaba wa mazao muhimu unaweza kufuata.

"Baada ya muda, kulingana na urefu na ukali wa vita hii, unaweza kuanza kushuhudia uhaba wa mizigo inayokuja katika bara la Afrika, na inaweza kusababisha uhaba. Hasa katika nchi za Kaskazini mwa Afrika, na kwa kiasi fulani katika Afrika Mashariki. ."

Aliongeza: "Kama ungeangalia bei ya chakula duniani, ilikuwa katika viwango vya juu zaidi mwanzoni mwa mwaka huu. Mgogoro huu tayari unaongeza mazingira hayo magumu kwa watumiaji wengi, hasa katika ulimwengu unaoendelea."

Siku ya Jumatatu, moja ya kampuni kubwa zaidi za mbolea duniani, Yara International, ilionya kwamba mzozo huo unaweza kuathiri sekta yake, na kuathiri zaidi bei ya chakula.

Bei ya mbolea tayari ilikuwa imepanda kutokana na kupanda kwa bei ya jumla ya gesi. Urusi pia inazalisha kiasi kikubwa cha virutubisho, kama potashi na fosfeti - viambato muhimu katika mbolea, ambavyo huwezesha mimea na mazao kukua.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here