Mvulana mmoja amewasili salama Slovakia baada ya kusafiri umbali wa kilomita 1,200 kutoka mashariki mwa Ukraine akiwa na mifuko midogo isiyozidi miwili, pasipoti na nambari ya simu ya jamaa zake.
Hassan, mwenye umri wa miaka 11, aliondoka nyumbani kwake huko Zaporizhzhia kwa sababu mama yake hangeweza kumwacha mama yake mzee.
Alimpandisha kwenye treni na hatimaye alipofika mpakani alisaidiwa kuvuka na maafisa wa forodha.
Maafisa walisema alikuwa shujaa wa kweli na alikuwa amewavutia watu wengi kwa tabasamu lake.
Kijana huyo alifika mpakani akiwa amebeba begi la plastiki, begi dogo jekundu na hati yake ya kusafiria. Alichukuliwa na watu waliojitolea ambao walimpa chakula na kinywaji huku maafisa wa mpakani wakiwasiliana na jamaa katika mji mkuu wa Slovakia Bratislava.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Mama yake, katika video iliyotumwa na polisi wa Slovakia, alishukuru kila mtu kwa kumtunza mwanawe na akaeleza kwa nini alisafiri kote nchini wakati ilikuwa katika mtego wa uvamizi wa Urusi.
"Karibu na mji wangu kuna kiwanda cha kuzalisha umeme ambacho Warusi wanarusha makombora. Sikuweza kumuacha mama yangu - hawezi kutembea peke yake - kwa hivyo nilimtuma mwanangu Slovakia," Julia Pisecka, ambaye ni mjane alisema.
Kituo cha nguvu za nyuklia huko Zaporizhzhia ndicho kikubwa zaidi barani Ulaya. Kilitekwa na jeshi la Urusi mwishoni mwa juma baada ya shambulio ambalo Rais Volodymyr Zelensky alionya kuwa lingeweza kusababisha uharibifu kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko maafa ya Chernobyl mnamo 1986.
Hassan ni mmoja wa zaidi ya watu milioni mbili waliokimbia vita vya Urusi nchini Ukraine. Zaidi ya milioni 1.2 wamewasili Poland, wakati 140,745 wamefika Slovakia, kulingana na takwimu za hivi karibuni za Umoja wa Mataifa.
Akizuia kutokwa na machozi, mama yake alisihi watoto wa Ukraine wapewe sehemu salama.
Afisa wa wizara ya mambo ya ndani ya Slovakia alisema Hassan amevutia kila mtu mpakani kwa tabasamu lake, kutoogopa na azma yake.
Afisa huyo alisema alikuwa ametumia nambari ya simu iliyoandikwa kwenye mkono wa mvulana huyo, pamoja na karatasi aliyokuwa nayo mfukoni, kuwasiliana na jamaa katika mji mkuu wa Slovakia waliokuja kumchukua.
Waziri wa Mambo ya Ndani Roman Mikulec alikutana na Hassan siku ya Jumatatu na kusema yeye na ndugu zake tayari walikuwa wameomba ulinzi wa muda nchini Slovakia.
Viongozi wa Slovakia waliwataka watu waliokuwa na nia ya kumsaidia mama na bibi wa kijana huyo kuchangia chama cha vijana wa Kislovakia cha ZKSM.
No comments:
Post a Comment