WAKURUGENZI HALMASHAURI WATAKIWA KUBORESHA OFISI ZA MAAFISA ARDHI - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Saturday 19 March 2022

WAKURUGENZI HALMASHAURI WATAKIWA KUBORESHA OFISI ZA MAAFISA ARDHI

 Wakurugenzi wa Halmashauri Nchini wametakiwa kutenga fedha zitokonazo na faida ya miradi ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi kuboresha ofisi za Maafisa Ardhi pamoja na kuwanunulia vifaa vya kisasa vitakavyosaidia kuaharakisha zoezi la kupanga, kupima na kumilikisha ardhi kwa ufanisi zaidi tofauti na sasa.


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ametoa agizo hilo kwa wakurugenzi hao leo mara baada Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii kupokea taarifa ya miradi ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi katika Halmashauri ya mji Bunda.

Halmashauri ya mji wa Bunda inatekeleza mradi huo katika vijiji tisa ambapo inakusudia kupima, kupanga na kumilikisha viwanja 7,450 baada ya kupokea mkopo wa Shilingi M.400.9 zinazotolewa na serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Naibu Waziri Kikwete aliongeza kuwa baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri wanawathamini Maafisa Ardhi wanapokuwa na fedha za miradi lakini miradi hiyo ikiisha wanawaweka kando ndio maana ofisi nyingi za maafisa hao ziko katika hali mbaya.

Naibu Waziri huyo pia aliungwa mkono na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Ally Makoa ambaye alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bunda Emmanuel Mkongo kuboresha Ofisi ya Maafisa ardhi kwa kutumia sehemu ya faida itakayopatikana kwenye mauzo ya viwanja mara baada ya kurejesha mkopo kwa Wizara ya Ardhi.

Ripoti ya mradi wa Kupanga, kupima na kumilikisha ardhi iliyotolewa na Mkurugenzi Halmashauri Mji Bunda Emmanuel Mkungo inasema bada ya kukamilisha zoezi hili inakusudia kukusanya Bil. 1.9 zitakazo tokana na mauzo ya viwanja hivyo.

Kufuatia makadilio hayo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Munge Ally Makoa akaishauri Halmashauri hiyo na nyingine zenye miradi kama hiyo kutumia sehemu ya faida hiyo kununua vitendea kazi vya maafisa ardhi na kuboresha miundombinu ya Ofisi zao.

‘’Haiwezekani kwa wanaokuletea kiasi hicho cha fedha kufanya kazi katika mazingira magumu wakati ofisi yako inatoa kipaumbele katika maeneo mengine.’’ Alisema Ally Makoa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Mali Asili na Utalii.

Mradi wa Kupanga, kupima na kumilikisha ardhi unaotekelezwa na Halmashauri Mji Bunda unafanyika katika vijiji tisa vya Mbugani viwanja 650,Shuleni viwanja 600,Katoriki viwanja 1,000, Ruselu viwanja 700, Kilimani 800, Zanziba 300, Balili 1, 200, Idara ya maji 2000 na Guta viwanja 200. Halmashauri ya mji Bunda inatekeleza zoezi la Kupanga, Kupima na Kumilikisha ardhi katika vijiji hivyo na tayari imeishatumia takriban M. 100 kwa zoezi linaloendelea na Serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi tayari imeisha toa Sh. Bil.50 kukopesha Halmashauri 55 nchini ikiwemo Chuo cha Ardhi Morogoro, Dar es Salaam na Tabora.

1.       Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akikagua vigingi vinavyotengenezwa na Halmashauri ya mji Bunda vitakavyotumika katika Mradi wa kupanga,kupima na kumilikisha ardhi.


1.       Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akitoa zawadi kwa Bi.Joyce Nyangoji baada ya kufuraishwa na namna anavyoweza kupanga vigingi kwa ustadi wakati wa ukaguzi wa  zoezi la kujenga vigingi vinavyotengenezwa na Halmashauri ya mji Bunda vitakavyotumika katika Mradi wa kupanga,kupima na kumilikisha ardhi.

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here