Mtayarishaji wa tuzo za Oscar amesema alizuia Will Smith "kuondolewa kwa lazima " kwenye sherehe hiyo kwa sababu "Chris Rock hakutaka hilo".
Will Packer alisema aliambiwa waandaji walikuwa na mpango wa kumfukuza muigizaji huyo baada ya kumpiga kibao mchekeshaji huyo jukwaani.
"Sikuwa sehemu ya mazungumzo hayo," Packer alisema.
"Kwa hivyo, mara moja nilienda kwa uongozi wa Chuo ambao walikuwepo na nikasema, 'Chris Rock hataki hivyo'."
Packer aliambia kipindi cha Good Morning America cha ABC, katika mahojiano yake ya kwanza tangu tukio hilo, kwamba alikuwa amewaambia wakuu wa chuo hicho: "Rock ameweka wazi kuwa hataki kufanya hali mbaya kuwa mbaya zaidi."
Aliongeza: "Hiyo ilikuwa nguvu ya Chris. Hakutaka kulipiza kisasi. Sauti yake haikuwa na hasira.
"Kwa hivyo nilikuwa nikitetea kile Rock alitaka wakati huo, ambayo haikuwa kumwondoa Will Smith wakati huo, kwa sababu, kama nilivyoelezewa sasa, hilo lilikuwa chaguo pekee wakati huo.
"Imeelezwa kuwa kulikuwa na mazungumzo ambayo sikuwa sehemu ya kumtaka aondoke kwa hiari."
Packer pia alieleza jinsi Rock aliwaambia maafisa wa polisi kwenye sherehe hiyo kuwa hataki Smith akamatwe.
"Walikuwa wakisema, unajua, hii ni – kumshambulia mtu -ndio neno walilotumia wakati huo. Walisema, 'Tutakwenda kumchukua. Tumejiandaa. Tumejiandaa kwenda kumchukua sasa hivi. Unaweza kumfungulia mashtaka. Tunaweza kumkamata'.
"Walikuwa wakiweka chaguo za hatua, na walipokuwa wakizungumza, Chris alikuwa akipuuza sana chaguzi hizo. Alikuwa akisema, 'Hapana, niko sawa.' Alikuwa kama, 'Hapana, hapana, hapana', hata mahali ambapo nilisema, 'Chris , Waache wamalize'.
"Maafisa wengine wa LAPD walimaliza kueleza hatua anazoweza kuchukua na wakasema, 'Je, ungependa tuchukue hatua yoyote?' Akasema, Hapana. Akasema, La.
Smith ameomba radhi kwa kumpiga Rock juu ya utani kuhusu mke wake, Jada.

No comments:
Post a Comment