Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linasema lori zake za chakula zimeingia katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi katika eneo lenye vita la Tigray nchini Ethiopia kwa mara ya kwanza tangu Desemba.
Makubaliano ya amani ya kibinadamu yalikubaliwa kati ya serikali na vikosi vya Tigray wiki iliyopita, lakini barabara zilikuwa zimefungwa huku pande zinazozozana zikishutumiwa kuhusu nani alaumiwe.
Malori hayo ya misaada yaliyobeba tani 500 za chakula na vifaa vingine yamevuka hadi katika maeneo yanayodhibitiwa na vikosi vya Tigray yanatarajiwa kuwasili katika mji mkuu wa eneo la Mekelle.
Afisa mkuu wa chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF), kundi lililokuwa na vita na serikali kwa muda wa miezi 17, ameitaja hatua hiyo "hatua katika mwelekeo sahihi".
Serikali - katika taarifa ya awali - ilikuwa imesema kuwa imejitolea kuwezesha upitishaji salama wa misaada.
Msaada huo wa chakula unatarajiwa kugawiwa kwa familia zilizoachwa kwenye ukingo wa njaa kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Lakini huku watu milioni sita mjini Tigray wakihitaji msaada na mamia ya maelfu wanakabiliwa na njaa, misaada zaidi inahitajika.
Ethiopia: Mzozo wa Tigray ulivyogeuka vita vya wenyewe kwa wenyewe
Vita vya Ethiopia: Kwanini kujua kinachoendelea Tigray ni muhimu?

No comments:
Post a Comment