Maandamano ya Zuma nchini Afrika Kusini yalilenga kuyumbisha uchumi - Ramaphosa - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 1 April 2022

Maandamano ya Zuma nchini Afrika Kusini yalilenga kuyumbisha uchumi - Ramaphosa

 

th

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameliambia jopo la uchunguzi kuwa ghasia na uporaji katika majimbo mawili makubwa Julai mwaka jana ulikuwa ni jaribio la makusudi la kuyumbisha uchumi.

Takriban watu 350 waliuawa katika ghasia hizo katika muda wa wiki moja huko KwaZulu-Natal na Gauteng baada ya Rais wa zamani Jacob Zuma kufungwa jela kwa kudharau mahakama.

Bw Zuma alihukumiwa kwa kukataa kwake kutoa ushahidi mbele ya tume ya ufisadi. Wafuasi wake walikuwa wakitaka aachiliwe.

Rais Ramaphosa aliambia uchunguzi wa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Afrika Kusini kwamba ingawa maandamano ya awali yaliwasilishwa kama malalamiko ya kisiasa, kwa kweli yalikuwa ni jaribio la kudhoofisha demokrasia ya nchi.

Machafuko mabaya zaidi tangu mwisho wa ubaguzi wa rangi yaligharimu uchumi $3.3bn (£2.5bn).

Miezi kadhaa baadaye, hakuna mtu mkuu aliyekamatwa. Bw Ramaphosa alisema uchunguzi wa kuwapata washukiwa wakuu bado unaendelea.

Ghasia Afrika Kusini: Uporaji na vifo vyaongezeka katika purukushani zilizoanza kama maandamano ya kumuunga mkono Zuma

Jacob Zuma: Rais wa zamani wa Afrika Kusini ambaye uongozi wake ulikumbwa na utata mwingi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here