
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku
Paris St-Germain wanahusishwa katika mazungumzo ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku mwaka mmoja tu baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 28 kuwagharimu Blues pauni milioni 98 kutoka Inter Milan. (But via Sun)
RB Leipzig wanajaribu kupata dau la meneja aliyeteuliwa na Manchester United Erik ten Hag kutoka Ajax kama meneja wao mpya . (Telegraph - subscription required)

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Haaland
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Haaland, 21,amepuuzilia mbali nia ya kujiunga na klabu ya Manchester United kwasababu mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway haamini kuwa wanaweza kutimiza matamanio yake ya ndani ya uwanja. (ESPN)

CHANZO CHA PICHA,REUTERS
Jesse Lingard
Roma, AC Milan na Juventus wamejiunga na West Ham pamoja na Newcastle katika kuelezea nia yao ya kusaini mshambuliaji wa Jesse Lingard, 29, wakati mkataba wake katika Manchester United utakapomalizika msimu huu. (Mirror)
Borussia Dortmund ndio wanaopendelewa katika kusaini mkataba na Mshambuliaji Mbelgiji Eden Hazard, 31, kutoka Real Madrid - na katika mbio hizo wako mbele ya Arsenal na AC Milan. (Cadena Ser - in Spanish)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Paul pogba
Manchester United wanapanga kukamilisha kupanga safu yao ya kati msimu huu, huku kiungo wa kati Mfaransa mwenye umri wa miaka 29 Paul pogba alitarajiwa kuondoka wakati mkataba wake utakapoisha mwezi Juni mwaka huu. (Mirror)
Fursa za Tottenham za kusaini mkataba na mlinzi Mcroatia Josko Gvardiol msimu huu "huenda zisifanikiwa kabisa" huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 akisema anafurahia kuwepo katika klabu ya Ujerumani ya RB Leipzig. (RB Live - in German)

CHANZO CHA PICHA,REX FEATURES
Mlinzi wa klabu ya Chelsea- Levi Colwill
Klabu kadhaa za Primia Ligi na Ulaya zinatarajiwa kuchukua hatua ya kumchukua mlinzi Muingereza anayechezea klabu ya Chelsea- Levi Colwill mwenye umri wa miaka 19, ambaye anacheza mchezo wa kufurahisha akiwa na mkataba wa mkopo hatika Huddersfield msimu huu. (Fabrizio Romano)
Chelsea wamewasiliana na mshambuliaji wa chuo cha Arsenal cha Khayon Muingereza Edwards juu ya uwezekano wa uhamisho, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 akiwa bado hajaamua mkataba wa kikazi na Gunners. (Goal)
No comments:
Post a Comment