Mapigano kati ya wachimba madini wasio rasmi katika sehemu ya mbali ya kaskazini mwa Chad yamesababisha takriban watu 100 kupoteza maisha na 40 kujeruhiwa, serikali inasema.
Kilichoanza kama "mzozo wa kawaida kati ya watu wawili... ulizidi na kuwa maafa", Waziri wa Ulinzi Daoud Yaya Brahim aliliambia shirika la habari la AFP.
Wilaya ya milima ya Kouri Bougoudi karibu na mpaka wa Libya inawavutia wachimba migodi kutoka ng'ambo ya Chad na majirani zake.
Mapigano hayo yalitokea wiki jana lakini maelezo yanajitokeza sasa hivi.
Baadhi ya makundi yameweka idadi ya vifo kuwa kubwa kuliko mamlaka, na wamelaumu vikosi vya usalama kwa idadi ya vifo hivyo.
Serikali ilituma ujumbe katika eneo lililoathiriwa - kama kilomita 1,000 (maili 620) kaskazini-mashariki mwa mji mkuu, N'Djamena - wakati habari za ghasia zilipokuja.

No comments:
Post a Comment