Uchaguzi Kenya 2022:Ukweli wa madai ya Raila Odinga kuhusu ufisadi wabainishwa - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 5 August 2022

Uchaguzi Kenya 2022:Ukweli wa madai ya Raila Odinga kuhusu ufisadi wabainishwa

 

Bw. Odinga na mgombea mwenza, Martha Karua, kwenye kampeni

CHANZO CHA PICHA,AFP

Aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga amekuwa akifanya kampeni ya kuchukua wadhifa wa rais kutoka kwa Uhuru Kenyatta. Amejikita katika masuala ya ufisadi kuwa jambo kuu katika mikutano na hotuba zake.

Hapo awali tulichunguza mgombea mwingine, William Ruto. Hapa tunaangazia baadhi ya madai yaliyotolewa na Bw Odinga.

'Ruto hana mgombea mwenza kwa sababu [Rigathi Gachagua]...amepatikana na hatia ya .... uhalifu mkubwa wa kiuchumi nchini'

Bw Gachagua, ambaye anafanya kampeni ya kuwa naibu rais pamoja na Bw Ruto, aliamriwa na mahakama mnamo Julai 28 kurejesha zaidi ya shilingi milioni 200 za Kenya (Ksh) ($1.7m, £1.4m) kwa sababu alishindwa kueleza jinsi alivyopata fedha hizo.Bw Gachagua anasema kwamba hakupewa nafasi ya kupinga ushahidi dhidi yake na kwamba atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Raila Odinga amemtaka ajiondoe kwenye uchaguzi huo, akisema kuwa kwa mujibu wa katiba ya Kenya "huwezi kugombea urais au kuwa mgombea mwenza wa urais ikiwa umefunguliwa mashtaka ya uhalifu".

"Anasema atakata rufaa," aliongeza Bw Odinga, "lakini jinsi mambo yalivyo leo anahukumiwa, na hatia kama alivyoshtakiwa."

Hata hivyo, kesi inayomhusisha Bw Gachagua ilikuwa ya madai iliyoletwa na shirika la kudhibiti mali nchini Kenya kwa madhumuni ya kurejesha mapato ya ufisadi. Haikuwa kesi ya jinai na tofauti ni muhimu.

Katiba inatamka kuwa mtu atapoteza sifa ya kushika nafasi ya rais, naibu wa rais au mbunge iwapo:

• amehukumiwa kwa takribani miezi sita jela

• Ametumia vibaya ofisi ya Umma

Lakini pia inasema haujakataliwa "isipokuwa uwezekano wote wa kukata rufaa au mapitio ya hukumu husika au uamuzi umekamilika."

Lakini pia inasema haupotezi sifa 'isipokuwa njia zote za rufaa au tathmini ya hukumu husika ama uamuzi zimetumika'

Mwanasheria wa Kikatiba Bobby Mkangi alituambia anaamini hii inaruhusu mtu kuendelea kugombea ofisi ya umma "wakati mchakato huu [wa rufaa] unaendelea."

Bw Gachagua pia anakabiliwa na kesi ya jinai ya ufisadi , lakini kesi hii haitasikilizwa hadi Septemba.

'Yeye [William Ruto] anachangia…sawa na shilingi milioni 100 kwa mwezi [kwa] harambee.... mshahara wake ukiwa ni shilingi milioni mbili pekee.'

Bw Odinga alisema katika mahojiano ya tarehe 21 Julai, lakini hatujui jinsi alivyofikia kiasi cha Ksh100m ($840,000, £690,000) kwa mwezi.

Bw Ruto ameshiriki katika hafla nyingi za kuchangisha pesa katika miaka ya hivi karibuni, lakini hakuna hitaji la kisheria nchini Kenya kwa wafadhili kutangaza michango yao. Mara tu kampeni za uchaguzi zikiendelea, hakuna mgombea anayeruhusiwa kutoa michango zaidi.

Nani yuko kwenye kinyang'anyiro cha kuiongoza Kenya ?

Fahamu zaidi kuwahusu wagombea urais wa Kenya

Chagua mgombea ili kutazama wasifu wake

Pata maelezo zaidi kuhusu sera za wagombea urais hapa

Tumeuliza ofisi ya Bw Odinga jinsi alivyoipata takwimu hiyo kwa jinsi Bw Ruto amechangia harambee hizi na lini alizifanya, lakini hatujapata jibu.

Kuhusu kiasi kilichotajwa cha mshahara wa kila mwezi wa Bw Ruto, Gazeti rasmi la Kenya limeorodhesha malipo yake kama Ksh1.2m ($10,000, £8,300).

Bw Ruto pia anajulikana kuwa na vyanzo vya binafsi vya mapato kutoka kwenye uwekezaji na maslahi ya biashara, lakini haijulikani anapata nini kutokana na haya.

Masanduku ya kura

CHANZO CHA PICHA,AFP

'Hakuna afisa aliyepatikana na hatia katika Ofisi ya Waziri Mkuu [chini ya Bw Odinga]'

Bw Odinga alitoa madai hayo katika mahojiano ya hivi majuzi na BBC alipoulizwa kuhusu wakati wake akiwa Waziri Mkuu kuanzia 2008 hadi 2013.

Mnamo 2010, kashfa ya ufisadi ilizuka iliyohusisha programu ya mahindi ya ruzuku.

Uchaguzi wa Kenya 2022: Vyama vinakuahidi nini?

Chagua suala ambalo linakuvutia

Sera za kila chama

  • Azimio La Umoja One Kenya Coalition

  • Roots Party of Kenya

  • Chama cha Agano

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here