ZAIDI YA VIJANA 150 KUTOKA MAENEO MBALIMBALI ARUSHA WANUFAIKA NA ELIMU YA UJASIRIAMALI - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 12 October 2022

ZAIDI YA VIJANA 150 KUTOKA MAENEO MBALIMBALI ARUSHA WANUFAIKA NA ELIMU YA UJASIRIAMALI

 

Mkuu wa mkoa wa Arusha ,John Mongela  akizindua rasmi kituo  cha ujasiriamali  na ubunifu kwa vijana cha Westerwelle Startup Arusha 
Baadhi ya washiriki wakishuhudia uzinduzi wa  kituo hicho kipya ya ujasiriamali  na ubunifu kwa vijana katika hafla iliyofanyika mjini hapa. 
……………………………..
Zaidi ya vijana 150 kutoka maeneo mbalimbali mkoani Arusha wamenufaika na kituo cha ujasiriamali  na ubunifu cha Westerwelle Startup Haus Arusha kwa kupatiwa elimu kuhusu maswala  ya ujasiriamali  na kuunganishwa na masoko ndani na nje ya nchi.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Meneja Mkuu wa  kituo hicho cha Westerwelle Startup Haus Arusha,Collins Kimaro wakati akizungumza  katika uzinduzi wa kituo hicho uliofanyika jijini Arusha.
Amefafanua kuwa, Westerwelle Foundation kutoka Ujerumani imeungana na Obuntu Hub kutoka Arusha kufungua kituo hicho  kikubwa kwa ajili  ya kuwasaidia vijana wajasiriamali Tanzania na kuweza kuanzisha shughuli  zao na kuondokana na changamoto ya ukosefu wa ajira. 
Kimaro amesema kuwa,uzinduzi wa kituo hicho cha ujasiriamali  na ubunifu kwa vijana kinalenga kuwasaidia vijana wajasiriamali Tanzania kwa lengo la kuchochea maendeleo kupitia  ujasiriamali. 
Amesema kuwa,Tanzania sasa inajiunga kwenye mtandao  huo wa kimataifa ambao tayari kuna kituo  Tunisia,Rwanda,ambapo malengo yao ni  kuongeza nchi moja  kila  mwaka.
Ameongeza kuwa, kituo hicho tayari kina programu 4 kwa ajili ya wajasiriamali  kwenye sekta za kilimo,utalii,uchumi wa  kidigitali  na mabadiliko ya tabia nchi kukiwa na lengo la kufikia vijana 5,000 ndani ya miaka mitano ijayo. 
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongela akizungumza  katika uzinduzi  huo amesema kuwa ,uwepo wa  kituo hicho utasaidia sana kuwaunganisha vijana na masoko ndani na nje ya nchi na kuweza kuanzisha biashara zao na kuondokana na changamoto ya ajira.
Mongela amewataka vijana hao  kutumia  kituo hicho  kupata fursa mbalimbali  kujikwamua kiuchumi na kuweza kuondokana na changamoto  mbalimbali z ajira. 
Amesema kuwa,kituo hicho kwa Arusha kinatoa  mafunzo kwa vijana wabunifu na wajasiriamali katika kuwapa nafasi za kufanyia  shughuli zao na kuwasaidia kupata rasilimali  mbalimbali. 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa  bodi ya Westerwelle Foundation ,Michael Mronz amesema kuwa wamefungua kituo hiki  nchini Tanzania kwa lengo la kuwawezesha vijana kuweza kunufaika na fursa nyingi .
Mronz amesema kuwa, Tanzania ina  fursa nyingi kutokana na uchumi  unaokuwa kwa kazi,nguvu kazi kubwa,utulivu wa kisiasa, na serikali yenye ushirikiano  mkubwa.
“Vituo  hivi vinalenga  kuwasaidia vijana kuweza kuwa wabunifu na kuendeleza  bunifu  zao  sambamba na kuwatafutia  masoko ndani na nje ya nchi na vijana wengi wameweza  kunufaika na kituo hiki  kwani kipo  nchini Kigali,Tunisia  na Tanzania hapa  Arusha,hivyo nawaomba sana vijana wajitokeze  kwa wingi kuchangamkia fursa  mbalimbali kupitia kituo hiki  cha kusaidia vijana katika maswala mbalimbali.”alisema  Mronz. 
Baadhi ya vijana wanaonufaika na kituo hicho ,Getruda  Mollel amesema kuwa,  kupitia kituo hicho wameweza kunufaika kwa  kuanzisha shughuli  mbalimbali sambamba na kupata fursa ya kuunganishwa  na masoko  ya nje ya nchi na kuwez kujikwamua  kiuchumi. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here