Hary Kane akifanya shambulio
Bado kuna nafasi nne za hatua ya kufuzu kwa 16 bora katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya tunapoingia katika awamu ya mwisho ya mechi za makundi - huku Tottenham Hotspur wakitafuta pointi wanayohitaji.
Manchester City na Chelsea wameshinda makundi yao, na Liverpool wamemaliza, lakini Spurs bado wana kazi ya ziada .
Kwa hivyo ni nani anahitaji nini, na ni nini kimeamuliwa?
Kundi A
Liverpool inahitaji kuifunga Napoli kwa mabao manne au zaidi ili kujikatia tiketi ya kushinda kundi A. Bila hivyo mabingwa ha owa Itli wataibuka mshindi katika kundi hilo.Ili Rangers waweze kumaliza kwenye nafasi ya Ligi ya Europa watalazimika kuifunga Ajax mabao matano au zaidi, vinginevyo watakuwa wametolewa katika kombe hilo.
Ligi ya Mabingwa hutumia mbinu ya matokeo baina ya timu mbilizi zilizokutana kabla ya tofauti ya mabao.
Kundi B
Club Bruges itashinda kundi iwapo itapata matokeo sawa na yale ya Porto . Ikiwa Porto watachukua pointi zaidi ya Bruges, watamaliza wakiwa juu.
Vile vile, Atletico itamaliza katika nafasi nzuri ya Ligi ya Europa isipokuwa iwapo Bayer Leverkusen itaboresha matokeo yao. Timu hiyo ya Ujerumani itamaliza ya tatu ikiwa itapata pointi zaidi ya Atletico.
Kundi C
Nafasi zote nne za kundi zimeamuliwa, ikimaanisha kuwa hakuna mechi itakayosababisha mabadiliko yoyote.
Kundi D
Kundi la karibu zaidi - pande zote nne zinajua ushindi utawaweka katika hatua ya mtoano. Timu yoyote inaweza kushinda kundi hili, ingawa Spurs wanajua wangefanya hivyo kwa ushindi.
Spurs na Sporting zinahitaji sare tu katika michezo yao ili kuvuka. Ikiwa Spurs itapoteza itamaliza nafasi ya tatu na kutolewa katika nafasi ya Ligi ya Europa.
Kundi E
Chelsea tayari wameshinda kundi hilo. Milan watakuwa katika nafasi ya pili wakiwa na sare au kushinda dhidi ya Salzburg, lakini timu hiyo ya Austria itachukua nafasi ya pili iwapo itaibuka mshindi.
Dinamo Zagreb bado wanaweza kumaliza katika nafasi ya kusalia Ligi ya Europa lakini watalazimika kuishinda Chelsea na kutumaini Salzburg itapoteza.
Kundi F
Dinamo Zagreb bado wanaweza kumaliza katika nafasi ya kusalia Ligi ya Europa lakini watalazimika kuishinda Chelsea na kutumaini Salzburg itapoteza.
Leipzig watafuzu hatua ya mtoano mradi tu hawatapoteza dhidi ya Shakhtar, lakini upande wa timu hiyo ya Ukraine watafuzu badala yake iwapo watashinda.
Real itamaliza kileleni ikiwa itaifunga Celtic, ambao watamaliza wakiwa chini hata iweje.
Kundi G
Nafasi zote nne za kundi zimeamuliwa, ikimaanisha kuwa hakuna mechi itakayobadilisha matokeo katika kundi hili.
Kundi H
Yeyote kati ya PSG na Benfica atatwaa pointi zaidi katika mechi zao za mwisho na kushinda kundi iwapo atashinda.
Iwapo watapata pointi sawa, tofauti yao ya mabao itaangaziwa kwa kuwa wako sawa katika matokeo ya mechi za ana kwa ana.









No comments:
Post a Comment