Ilkay Gundogan
Manchester City wanahofia Ilkay Gundogan ataondoka katika klabu hiyo kwa uhamisho wa bila malipo msimu ujao. Kiungo huyo wa kati wa Ujerumani, 32, bado hajakubali mkataba mpya, na mkataba wake wa sasa unamalizika Juni. (Football Insider)
Manchester United wanataka kupata hatima ya Marcus Rashford Old Trafford kabla ya mwisho wa mwaka ili kumzuia kunyakuliwa. Mshambulizi huyo wa kimataifa wa Uingereza, 25, atakuwa huru kufanya mazungumzo na vilabu vya kigeni mwezi Januari isipokuwa iwapo atatia saini mkataba mpya au kipengele cha chaguo la mwaka mmoja katika kandarasi yake. (Daily Mail)
Manchester United wana nia ya kumsajili beki wa kulia wa Uingereza Max Aarons, 22, kutoka Norwich ili kumpa changamoto mchezaji wa kimataifa wa Ureno Diogo Dalot, 23, huku Mholanzi wa Bayer Leverkusen Jeremie Frimpong, 21, akiwa chaguo lingine. (Sun)
Rushford
Arsenal wameripotiwa kutuma maskauti kumtazama kiungo wa kati wa Palmeiras na Brazil Danilo wiki iliyopita, huku The Gunners wakiwa na nia ya kumleta mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 mwezi Januari. (Sun)Arsenal pia wanaripotiwa kufanya mazungumzo na winga wa Uruguay Facundo Torres, 22, kutoka Orlando City. (Evening Standard)
Manchester United bado wana nia ya kumsajili winga wa PSV Cody Gakpo, 23, huku Mholanzi huyo akikaribia kusajiliwa na Red Devils msimu wa joto. (GiveMeSport)
Gapko
Chelsea wanafikiria kumnunua mlinzi wa Wolves na Ureno Nelson Semedo, 28, kuchukua nafasi ya mchezaji wao wa kimataifa wa Uingereza aliyejeruhiwa Reece James, 22. (Express)
Brighton boss Roberto de Zerbi is keen to sign Ukraine centre-back Mykola Matviyenko, 26, who is valued at around £17.2m by Shakhtar Donetsk. (Athletic - subscription required)
Kiungo wa kati wa Flamengo wa Brazil Joao Gomes anasema Liverpool ni timu ambayo angeichezea, ingawa Real Madrid pia wanaripotiwa kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (ESPN - in Portuguese)
de Jong
West Ham wanamfuatilia Isaiah Jones wa Middlesbrough, huku winga huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 23 akivutia pia Crystal Palace. (GiveMeSport)
Kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong anataka kusalia katika klabu hiyo ya Catalan licha ya Manchester United kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Sport)
Juventus wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 27, kutoka Lazio na mlinzi wa Italia Alessandro Bastoni, 23, kutoka Inter Milan ili kujaribu kumpata mkufunzi wa Tottenham Antonio Conte kurejea katika klabu hiyo. (Calciomercato)
Saliba
Arsenal wamempa mlinzi wa Ufaransa William Saliba, 21, mkataba mpya. (Athletic - subscription required)
Leicester hawafikirii kumuuza kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans mwezi Januari huku kukiwa na ripoti kwamba Arsenal bado wana nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.. (90min)





No comments:
Post a Comment