Tetesi za soka Ulaya Jumatano 28.12.2022 - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Tuesday, 27 December 2022

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 28.12.2022

 


Pickford

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Everton bado hawajasaini mkataba wa miaka mitano ambao wamekubaliwa na kipa wa England Jordan Pickford, 28, na hilo limewaweka mguu sawa Chelsea, Manchester United na Tottenham. (Mail)

Arsenal wameweka ofa ya pauni milioni 55 kwa winga wa Ukraine Mykhaylo Mudryk iliyokataliwa na Shakhtar Donetsk lakini wanatarajiwa kupeleka ofa mpya kwa ajii ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Evening Standard)

Tottenham wanatarajiwa kuvunja rekodi ya uhamisho wa mchezaji wa kike katika Ligi Kuu ya Wanawake baada ya mshambuliaji England Beth England, 28, kukubali kujiunga nao kwa £250,000 kutoka Chelsea. (Mail)

Real Madrid wanapanga kumnunua beki wa pembeni wa Bayern Munich na Canada Alphonso Davies, 22. (AS - in Spanish)

Davies

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Alphonso Davies

Manchester United wanaangazia usajili wa mkopo ili kuongezea nguvu safu yao ya ushambuliaji mnamo Januari baada ya kuvuka bajeti yao wakati wa majira ya joto walipotumia zaidi ya pauni milioni 200. (Telegraph)

Newcastle United inaweza kujaribu kumsajili kiungo wa kati wa Italia Jorginho mwenye umri wa miaka 31 msimu wa joto wakati mkataba wake unamalizika Chelsea, ambao wanafikiriwa kumtaka kiungo wa kati wa Benfica na Argentina Enzo Fernandez, 21. (Mail).

Mshambulizi wa Lille Jonathan David amehusishwa na klabu za Chelsea na Manchester United na mchezaji huyo wa kimataifa wa Canada mwenye umri wa miaka 22 anasema "kila mchezaji angependa kucheza" katika Ligi kuu England "siku moja". (La Voic du Nord, via Metro)

David

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Jonathan David

Mlinzi wa Liverpool Virgil van Dijk alizungumza na mchezaji mwenzake wa Uholanzi Cody Gakpo kusaidia kumshawishi mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kujiunga na Liverpool (Reds) akitokea PSV Eindhoven, na makubaliano yakiwa yamefikiwa kati ya klabu hizo mbili. (Eindhovens Dagblad, via Mail)

Leeds United wanatayarisha ofa kwa mlinzi wa Red Bull Salzburg na Austria Maximilian Wober, 24. (Fabrizio Romano)

Kocha wa zamani wa Fulham na Bournemouth Scott Parker ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kuwa meneja mpya Norwich City, ambao wamemtimua Dean Smith. Aliyekuwa meneja wa Burnley Sean Dyche pia yuko katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi hiyo.

Parker

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Scott Parker

Atletico Madrid na Sevilla wana nia ya kumsajili beki wa kati wa Argentina Nicolas Otamendi, 34, ambaye kandarasi yake itamalizika Benfica msimu wa joto. (Football Espana)

Inter Milan wanajaribu kupambana na ushindani kutoka kwa vilabu kadhaa vya Premier League kwa mshambuliaji wa Borussia Monchengladbach na Ufaransa Marcus Thuram, 25. (90min).

No comments:

Post a Comment