Maafisa wa shirika la anga wanasema ni ajali mbaya kutokea nchini humo tangu miongo mitatu iliyopita katika taifa hilo la Himalaya.
Maelfu ya waokozi walizunguuka eneo hilo la milima kwa ajili ya kutoa msaada katika ajali ya nsdege ya Yeti iliyokuwa imebeba abiria 72 kutoka mji mkuu Kathmandu.
Televisheni za ndani zimeonyesha picha wafanyakazi wakifanya shughuli za uokozi katika ndege hiyo iliyokatika vipande baada ya kupata ajali.
Data za shirika la anga zinaonyesha kuwa Nepal iliwahi kukabiliwa na ajali ya ndege iliyokuwa na vifo mwaka 1992 wakati ndege ya kimataifa ya Pakistan, Airbus300 ilipoanguka upande wa mlima ilipokuwa inakaribia kutua Kathmandu na kusababisha vifo vya watu 167 waliokuwemo ndani.
Ndege iliyopata ajali Jumapili ilifanya mawasiliano na mamlaka za uwanja wa ndege kutoka Seti majira ya asubuhi, shirika la anga limesema katika taarifa yake ya maandishi, na baadae ikaanguka.
Afisa wa polisi Ajay K.C amesema wafanyakazi wa uokozi walikuwa na wakati mgumu kujaribu kufikia eneo kati ya milima miwili karibu na mji wa kitalii karibu na uwanja wa ndege.
Serikali imeunda jopo la uchunguzi kujua chanzo cha ajali na inatarajia kupata ripoti ndani ya siku 45, waziri wa fedha Bishnu Paudel amewaambia waandishi wa habari.