Watu 5 wamekufa katika shambulio la bomu Congo - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 16 January 2023

Watu 5 wamekufa katika shambulio la bomu Congo

 

Jeshi la Congo limesema takriban watu 5 wamekufa katika shambulizi la bomu linaloshukiwa kutekelezwa na wanamgambo wa kiislamu wenye msimamo mkali wakati wa ibada ya Jumapili , kwenye kanisa la Protestant mashariki mwa mji wa Kasindi unaopakana na Uganda. Msemaji wa jeshi Anthony Mualushay ameliambia shirika la habari la Reuters kwa njia ya simu. Amesema wakati wa ibada ya jumapili inashutumiwa kuwa kundi la ADF kutoka Uganda ndio limehusika na shambuklizi hilo. “Licha ya kuwepo hatua za usalama zilizowekwa, ishara ya kwanza inaonesha kuwa ADF iko nyuma ya shambulizi hili, Anthony Mualushay alisema kwa njia ya simu.”

Hata hivyo kundi hilo la ADF halikupatikana ili kutoa maelezo , na halijatoa taarifa kuhusika na shambulizi hilo. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa ADF kushambulia Kasindi tangu kundi hilo lilipoongeza mashambulizi yake katika eneo hilo mwaka 2014 , mratibu wa ndani wa eneo hilo Charles Omeonga ameiambia Reuters , ambapo amekadiria vifo vinaweza kufika 10. Kasindi iko katika jimbo ambako vikosi vya Congo na Uganda vimeanzisha kampeni za mashambulizi dhidi ya ADF ambayo yalianza kama vuguvugu uganda lakini yamekuwepo zaidi Congo tangu miaka ya 1990. Liliahidi kuwa tiifu kwa kundi la Isamic state katikati mwa mwaka 2019 na linashutumiwa kuwauwa mamia ya wanakijiji wakati wa uvamizi wake wa mara kwa mara katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here