Maamuzi ya kuanzisha tasisi ya Fedha ya Afrika Mashariki – Benki Kuu ya Afrika Mashariki – yatafanyika mwaka huu wa 2023, jambo kuu linalohitajika katika utekelezaji utaratibu wa kuwa na sarafu moja.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt Peter Mathuki, alisema Baraza la Mawaziri linatarajiwa kupanga juu ya eneo itakapo kuwa taasisi ya EAMI mwaka huu.
Katika miaka ya karibuni, nchi wanachama zimekuwa zikiwania kuwa wenyeji wa EAMI, kila mmoja akijipanga kutumia fursa nyingi zilizoko kuvutia uwekezaji wa kigeni na kuwa kitovu cha kifedha katika kanda hiyo.
“EAMI itaundwa mwaka huu , kwa kile kitakacho ziwezesha mataifa wanachama kuunganisha sera zao za fedha na mapato, halafu baada ya miaka kama mitatu tutaweza kuwa na sarafu ya pamoja, ” aliwaambia waandishi wa habari wiki iliyopita.
Sarafu moja ya Afrika Mashariki itarahisisha biashara na watu kusafiri ndani ya eneo hilo, kitu ambacho kitafanikisha lengo la jumuiya la kuwa na soko la pamoja kama ilivyokusudiwa.
EAC ina jumla ya watu millioni 300, pamoja na wawekezaji kutoka nchi mbalimbali za dunia ambao watafaidika na soko hilo ambalo linawaunganisha wafanyabiashara kuwafikia watu wote barani Afrika.
Sarafu ya Afrika Mashariki, imekamilisha nguzo ya tatu ya muingiliano katika EAC baada ya kuundwa kwa umoja wa forodha na itifaki ya soko la pamoja ambazo ziliongeza ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama.
Chanzo cha habari hii ni gazeti la "The East African" linalochapishwa nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment