Makampuni ya nchi 13 yadaiwa kusaidia Myanmar kutengeneza silaha - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 16 January 2023

Makampuni ya nchi 13 yadaiwa kusaidia Myanmar kutengeneza silaha

 



Makampuni kutoka nchi 13 yameisaidia Myanmar, kujijengea uwezo wake wa kuzalisha silaha ambazo zinatumika kufanya ukatili kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya 2021, wataalam huru wa kimataifa wamegundua.

Ripoti iliyotolewa Jumatatu na Baraza Maalum la Ushauri la Myanmar inaeleza jinsi nchi hiyo imeongeza uzalishaji wa silaha tangu jeshi lichukue mamlaka Februari 1, 2021, na kusababisha vuguvugu kubwa la upinzani wa umma.

Mapinduzi ya kijeshi dhidi ya viongozi wa kiraia waliochaguliwa yaibadilisha karibu muongo mmoja wa maendeleo ya kuelekea demokrasia baada ya miaka 50 ya utawala wa kijeshi.

Chama cha msaada kwa wafungwa wa kisiasa wameandikisha zaidi ya vifo 2,700 vya raia katika ghasia ikijumuisha watoto 377 huku watu zaidi ya 13,000 wakishikiliwa. Inaaminika idadi ni kubwa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here