Uturuki wataka Sweden na Finland wawarudishe magaidi ili kupitisha maombi ya NATO - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 16 January 2023

Uturuki wataka Sweden na Finland wawarudishe magaidi ili kupitisha maombi ya NATO

 


Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema Sweden na Finland lazima ziwarudishe magaidi takriban 130 Uturuki kabla ya bunge lake halija pitisha mapendekezo yao ya kujinga na NATO.

Mataifa hayo mawili ya Kinordi mwaka jana yaliwasilisha maombi ya kujiunga na NATO baada ya Russia kuivamia Ukraine, lakini maombi yao lazima yapitishwe na wanachama 30 wa NATO.

Uturuki na Hungaru bado hazijapitisha maombi ya mataifa hayo mawili.

Uturuki imesema Sweden lazima ichukuwe hatua ya wazi dhidi ya kile inachokiona magaidi hasa wanamgambo wa Kikurdi, na kundi ambalo linalaumiwa na jaribio la mapinduzi la mwaka 2016.

Erdogan alisema kwamba kama magaidi hao hawatawasilishwa kwao basi hawata pitisha maombi ya nchi hizo mbili kupitia bunge la Uturuki.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here