Justin Welby anawakosoa makasisi wa Uganda kwa kuunga mkono sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 9 June 2023

Justin Welby anawakosoa makasisi wa Uganda kwa kuunga mkono sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja

 

Askofu Mkuu wa Canterbury ameeleza "huzuni na kufadhaika"


Kiongozi wa kiroho wa Kanisa la Anglikana amewataka makasisi nchini Uganda kukataa sheria mpya ya kupinga mapenzi ya jinsi moja ambayo imeidhinishwa na Rais Yoweri Museveni.

Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby, alisema hakuna uhalali kwa Waanglikana kuunga mkono sheria inayoenda kinyume na mafundisho ya Kikristo.

Kiongozi wa Ushirika wa Kianglikana duniani kote alisema amemwandikia Stephen Kaziimba, mkuu wa kanisa hilo nchini Uganda, kueleza "huzuni na masikitiko yake" kwamba kanisa limeunga mkono sheria.

Mapenzi ya jinsi moja sasa yanaadhibiwa kwa kifungo cha maisha jela, wakati kile ambacho sheria inakiita "mapenzi ya jinsi moja yaliyokithiri", ikiwa ni pamoja na kusambaza VVU, hupelekea hukumu ya kifo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here