Nahodha wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars Michael Olunga
Nahodha wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, Michael Olunga amehusishwa na ripoti kadhaa kuhusu kuhamia Ligi Kuu ya Uingereza lakini akasema atalizungumzia suala hilo hivi karibuni, na hivyo kuibua tetesi za uwezekano wake kuondoka Al Duhail.
Klabu ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza imeripotiwa kufuatilia hali ya mfungaji huyo wa magoli kutoka Kenya. {Echo Liverpool}.
Declan Rice
Arsenal itaongeza juhudi za kumnunua Declan Rice kwa pauni milioni 92 kwa matumaini kwamba kiungo huyo wa West Ham na Uingereza, 24, anaweza kujiunga kwa wakati kwa kabla ya kuanza kwa msimu. (Telegraph - usajili unahitajika)
Joao Palhinha
West Ham wanapania kumleta kiungo mkabaji wa Fulham na Ureno Joao Palhinha, 27, kuchukua nafasi ya Rice, huku Manchester City na Kalvin Phillips wa Uingereza na kiungo wa kati wa Southampton na England James Ward-Prowse pia wakiwa kwenye orodha hiyo. (Mail)
Mateo Kovacic
Kiungo wa kati wa Chelsea na Croatia Mateo Kovacic, 29, amekubali masharti ya kibinafsi na Manchester City baada ya kupiga hatua katika mazungumzo ya usajili. (Fabrizio Romano)
Liverpool wamepanga mazungumzo na wawakilishi wa kiungo wa Borussia Monchengladbach Mfaransa Manu Kone, 22. (Fabrizio Romano)




No comments:
Post a Comment