AKIBA COMMERCIAL BANK PLC YAANDAA JUKWAA LA WATEJA MKOANI MBEYA ZAIDI YA WATEJA 150 WASHIRIKI. - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Thursday, 19 June 2025

AKIBA COMMERCIAL BANK PLC YAANDAA JUKWAA LA WATEJA MKOANI MBEYA ZAIDI YA WATEJA 150 WASHIRIKI.

Tanzania – 18 Juni 2025 – Akiba Commercial Bank Plc (ACB) iliandaa mkutano Maalum wa Wateja jijini Mbeya lililowakutanisha zaidi ya wateja 150 kutoka sekta mbalimbali, kwa lengo la kuimarisha mahusiano na kuwataarifu wateja kuhusu maendeleo ya Benki pamoja na fursa mbali mbali za kuwainua wateja kiuchumi.Jukwaa hili lililenga kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya hivi karibuni ya benki, hususan katika huduma za kidijitali na maboresho ya uzoefu wa wateja. Aidha, lilitumika kama jukwaa la kutoa elimu ya kifedha kwa wateja ili kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi ya kifedha. Wateja walishiriki kikamilifu kwa kutoa maoni, mrejesho na mapendekezo kuhusu huduma za benki.


Benki ilitumia fursa hiyo kusikiliza, kujifunza na pia kutoa shukrani kwa wateja wake kwa uaminifu na ushirikiano wao wa muda mrefu. Akizungumza katika tukio hilo, Bi. Wezi Mwazani, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya Akiba, alitoa pongezi kwa mwitikio mkubwa na kusema: "Mwonekano wa ushiriki huu mkubwa unatupa faraja kuwa wateja wetu wanatuamini na wamechagua Akiba kama Benki yao pendwa. Hatuchukulii jambo hili kuwa la kawaida, na tunaendelea kujitolea kuwahudumia kwa ubora siku zote.


" Bw. Ntupa, Kiongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Soko la Mbeya, alipongeza juhudi za Benki kwa kuandaa jukwaa lenye maana kubwa, hasa kwa kuweka kipaumbele kwenye elimu ya kifedha. "Majukwaa kama haya ni muhimu kwa maendeleo ya biashara, yanatoa maarifa kwa wateja wetu na kuimarisha uhusiano wa kuaminiana kati ya benki na jamii ya wafanyabiashara," alisema Bw. Mtupa. Akihitimisha tukio hilo,
Afisa Biashara Mkuu wa Akiba Commercial Bank Plc Bi. Wezi Mwazani akifungua mkutano wa wateja ulioandaliwa na benki hiyo mkoani mbeya.

Bw. Humphrey Nyandidi, Meneja wa Tawi la Mbeya, alishukuru wateja kwa ushirikiano wao na kuahidi kuendelea kuwahudumia kwa bidii na kujituma. "Tunathamini sana uaminifu wenu, na tunaahidi kuendelea kuwahudumia kwa ari na moyo wa dhati ili kutimiza matarajio yenu na hata kuvuka kiwango hicho," alisema. Jukwaa hili la wateja ni sehemu ya mkakati mpana wa Benki ya Akiba wa kuimarisha mahusiano na wateja wake kupitia majukwaa ya majadiliano na mirejesho kutoka kwa wateja. Benki inaendelea kujikita katika kutoa huduma shirikishi za kifedha pamoja na elimu ya fedha.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here