Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL
MAKONDA amejitolea kumsaidia Kijana AHMED ALBAITY anaesumbuliwa na
tatizo la Uti wa Mgongo lililompelekea kulala kitandani kwa takribani
miaka 10.
AHMED ALBAITY anatakiwa kwenda kutibiwa
Nchini China kwa muda wa Wiki tatu akiambatana na Wasaidizi Wawili
ambapo Gharama za Matibabu zinazohitajika ni zaidi ya Dola 40,000 za
Marekani ambapo Sindano moja aliyoandikiwa inagharimu kiasi cha Dolla
27,000.
RC MAKONDA amesema atafanya jitihada
zote kuhakikisha AHMED anapatiwa Matibiwa ili aweze kupona na kutimiza
ndoto zake akiwa na Afya Njema.
Mapema leo RC MAKONDA ametembelewa
Ofisini kwake na Balozi Mpya wa China Nchini Tanzania Bi. WANG KE ambae
amekuja kujitambulisha kwa Mkuu wa Mkoa ambapo katika Mazungumzo RC
MAKONDA amemgusia Balozi huyo Suala la Matibabu ya AHMED ALBAITY ambapo
Balozi WANG KE alieambatana pia na Daktari Bingwa wa China aliebaki
Nchini kwaajili ya Shughuli ya Serikali ya China ambapo wamemtazama na
kupitia Ripoti ambapo wameahidi kulifanyia kazi suala hilo.
Katika Mazungumzo hayo pia wamejadili
Masuala mbalimbali ikiwemo Kuimarisha Usalama, Kampeni ya Ujenzi wa
Ofisi za Walimu na kuongeza huduma kwa Wananchi.
MAKONDA pia ameishukuru Serikali ya
China kwa kuleta Meli ya Jeshi la China yenye Hospital ndali ambayo
imesaidia kutoa vipimo na Matibabu kwa wananchi wengi.
Kwa Upande wake Bolozi Mpya wa China
Nchini Tanzania WANG KE amesema Serikali ya China itaendelea kusaidiana
na Tanzania katika masuala yote ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment