Yule daktari bingwa wa magonjwa ya
binadamu aliyejizolea umaarufu mkubwa hapa nchini siku za hivi karibuni
kufuatia kufika dau wakati wa mnada majumba bilionea Lugumi yaliyopo
jijini Dar es Salaam, Dkt. Louis Shika ametamba kuwa atafanya kweli
katika event ya Usiku wa 900 Itapendeza.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es
Salaam leo, Novemba 30, 2017, Dk Shika alisema; “Ninatarajia usiku wa
900 Itapendeza nitaongea na wakazi wa Dar es Salaam, tutazungumza mengi,
nawaomba wajitokeze, nimejiandaa vyema, karibuni nyote tuzungumze,
itapendeza mkifika nyote,” alisema Dkt. Shika.
Aidha katika hafla hiyo itakayofanyika
Desemba 9, 2017 katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo
Mbagala Zakhiem jijini Dar, burudani kibao zitapigwa zikiwemo kutoka
kwenye bendi za Twanga Pepeta, Jahazi Modern Taarabu, wasanii wa Bongo
Fleva na mchekeshaji maarufu nchini, Mc Pilipili.
Dk Shika anatarajiwa kufunguka mengi
ikiwemo maisha yake aliyoyapitia, masomo ya udaktari, maisha yake nchini
Urusi hadi aliporudi Tanzania pamoja na kutoa hamasa kwa vijana
hususani katika mambo ya ujasiliamali.

No comments:
Post a Comment