Zaidi ya raia 100 kutoka Ghana walikuwa
wanazuiliwa nchini Libya, wamerudi makwao baada ya Serikali kupata ndege
ya kuwapeleka nyumbani.
Walienda Libya wakiwa na matumaini ya kufika Ulaya lakini wakasalia kuwekwa katika vituo vya kufungwa kama wahamiaji haramu.
Kurudi kwao kulifuatia hamaki iliyotanda
dunia nzima baada ya kanda ya video kuibuka iliyoonyesha Waafrika
wakiuzwa kama watumwa nchini Libya.
Viongozi kutoka Afrika na Ulaya wamekuwa
wakijadiliana suala hilo katika mkutano nchini Ivory Coast na wameandaa
mpango wa pamoja ili kujaribu kutatua shida hiyo
No comments:
Post a Comment