Marekani imeyataka mataifa yote kukatiza
uhusiano wa kidiplomasia na ule wa kibiashara na Korea Kaskazini baada
ya taifa hilo kufanyia jaribio la kombora lake la masafa marefu.
Akizungumza katika baraza la usalama la
umoja wa kimataifa ,mjumbe wa Marekani katika baraza hilo Nikki Haley
amesema kuwa rais Trump amemtaka mwenzake wa China kukata usambazaji wa
mafuta kwa Pyongyang.
Amesema kuwa Marekani haitaki mzozo lakini Korea Kaskazini itaangamizwa iwapo vita vitazuka.
Onyo hilo linajiri baada ya Pyonyang kufanyia majaribio kombora lake la kwanza katika kipindi cha miezi miwili.
Korea Kaskazini imesema kuwa kombora
hilo lililorushwa siku ya Jumatano ambalo inasema liliruka kimo cha
kilomita 4,475, ikiwa ni mara kumi zaidi ya kimo cha kituo cha angani.
Madai hayo hayakuthibitishwa na wataalam wametiliashaka uwezo wa taifa hilo kuwa na teknolojia kama hiyo.
Hatahivyo kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema kuwa uzinduzi wa kombora hilo ulikuwa wa kufana.
Jaribio hilo likiwa mojawapo ya
majaribio yaliofanywa na taifa hilo limeshutumiwa na jamii ya kimataifa
na tayari baraza la usalama la umoja wa kimataifa limeitisha kikao cha
dharura.
Bi Haley alionya kuwa kuendelea kwa uchokozi kunalenga kuliyumbisha eneo hilo.
''Tunahitaji China kuchukua hatua zaidi'', alisema.
Rais Trump alimpigia simu rais Xi
Jinping mapema siku ya Jumatano , Ikulu ya Whitehouse ilisema kuwa rais
Trump alizungumza na Xi Jinping kwa simu akimtaka kuchukua hatua zozote
kuishawishi Korea Kaskazini kusitisha uchokozi na kusitisha mpango wake
wa kinyuklia

No comments:
Post a Comment