
- KAMPUNI ya Udalali ya YONO Auction Mart Ltd inatarajia kurudia mnada upya wa kuuza majengo ya Mfanyabiashara Said Lugumi ili kufidia deni la Serikali,ambapo Mnada huo unarudiwa upya baada kufanyika Mara mbili bila kufikia bei elekezi Wateja ambapo kila mteja alifika na bei yake.
- Mapema leo hii, akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar as Salaam ,Mkurugenzi wa Kampuni ya YONO Scholastika Kevela , amesema mnada huo ulifanyika kwa Mara ya TATU ulihusisha nyumba iliyopo Mbweni JKT wilayani Kinondoni na nyingine Upanga Wilayani Ilala.
- Kevela amesema kabla kuanza kwa mnada huo shart la kwanza waliloweka kila mteja anasajiliwa katika daftari maalum kisha kulipa fedha taslimu sh.milioni mbili.
-
- "Nyumba ya Mbweni JKT walijitkeza wateja watatu na bei ya mwisho waliofika ni sh.milioni 510 na nyumba ya Upanga walijitokeza Wateja wafanyabiashara ambao walifikia bei ya sh, milioni 650 kiwango cha bei elekezi akijafika" amesema Kevela.
-
- Kevela amesema kuwa, viwango hivyo vyote ambavyo wamefika Wateja havilingani na bei ambayo Serikali wamepanga hivyo mnada utafanyika tena mpaka sasa bado kuuzwa, huku akikataa kuviweka wazi viwango vilivyofikiwa na wateja n kudai kua kufanya hivyo ni ouvunja sheria za mnada.
-
- Aidha amesema kuwa, mnada huo unaofanywa na kampuni ya YONO kwa idhini ya Serikali ambayo ilipewa jukumu na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufidia deni la Serikali la sh .bilioni 14 .
-
- Awali minada iliyopita Ulifanyika Septemba 9 mwaka huu ambapo kampuni hiyo ilifanikiwa kuuza nyumba ya Upanga kwa sh .milioni 700 hata hivyo Serikali haikuridhika na bei hiyo na kuamua kufanya tathimini upya ili iuzwe tena.
-
- Pia mnada wa pili ulifanyika novemba 9 mwaka huu na Dkt. shika alifanikiwa kununua nyumba zote kwa gharama ya sh. Bilioni 3.2 nyumba ya kwanza ya .mbweni JKT kitalu Namba 57,yenye ukubwa wa mita za mraba 1,500 iliuzwa kwa sh,bilioni 1.1 iliyofuata kitalu Namba 47 yenye mita za mraba 1,500 iliuzwa kwa sh.milioni 900 Nyumba ya upanga iliyopo kitalu Namba 701 yenye ukubwa wa mita za mraba 400 iliuzwa kwa sh. milioni 1.2 hata hivyo Dtk. Shika alishindwa kulipa asilimia 25 ya fedha zote ambazo ni sh. milioni 800 hatua iliyosababisha akamatwe na kuwekwa ndani.
-
- Amewema kuwa kwa sasa wanajipanga tena kwa ushirikiano na TRA wawatoa taarifa rasmi siku ya kurudia kununua majengo hayo ya Mfanyabiashara Said Lugumi.
No comments:
Post a Comment