Maneno ya shombo ya wachezaji wa Manchester City, ndiyo yaliyosababisha mzozo na wenyewe kutwangana ngumi.
Hali
ya wachezaji hao kutoelewana imeelezwa ilisababishwa na kauli iliyotoka
katika kundi la wachezaji wa Man City waliokuwa wakipita mbele ya
wachezaji wa Man United baada ya kushinda 2-1.
Mmoja wa wachezaji alimueleza Zlatan Ibrahimovic kwamba: “Zlatan, unachonga sana lakini hauna unalofanya.”
Ilikuwa
tayari mchezo umeisha na baada ya hapo, ugomvi mkubwa uliibuka na
kusababisha Kocha Msaidizi wa Man City, Mikel Arteta kupasuliwa katika
paji la uso.
Man City ilifafanikiwa kutoka nyuma na kusawazisha mwisho kupata ushindi wa mabao 2-1.

No comments:
Post a Comment