Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Yanga
inaendelea kujifua kuhakikisha inatetea taji lake la Ligi Kuu Bara, sasa
ikiwa katika nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam FC.
Yanga haijawa na mwendo mzuri sana lakini wachezaji wake wameonekana kupania kubadili mambo wakiwa na juhudi kubwa mazoezini.

No comments:
Post a Comment