Vijana wa JKT wadaiwa kuua - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 16 December 2019

Vijana wa JKT wadaiwa kuua



Baadhi ya Vijana wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Kikosi cha Milundikwa Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa wanadaiwa kuvamia Kijiji cha Kipande na kutembeza kipigo kikali kwa Wananchi hadi mmoja wao Sabato Mbalamwezi kupoteza maisha .
Inaelezwa kuwa Sabato Mbalamwezi na mwenzie Renatus Wankamba walikamatwa na kuhifadhiwa Kituo cha Polisi kwa tuhuma za kuiba simu yenye thamani ya Tsh 25000, na wakiwa kituoni hapo walifika Vijana watano wa JKT na kuanza kuwaadhibu wakiwatuhumu kuwa wameiba simu ya mwenzao mmoja, Sabato alizidiwa baada ya kipigo na akafariki muda mfupi baada ya kukimbziwa Zahanati.
Wanakijiji walichukizwa na tukio hilo na kuanza kuwashambulia JKT hao hadi mmoja akakimbizwa Hospitali.
Kamanda wa Polisi Rukwa Jutine Masonje amesema Vijana watano wa JKT waliosababisha kifo cha Mbalamwezi wanashikiliwa na Polisi kwa mahojiano na watafikishwa Mahakamani, pia Wanakijiji 35 waliofanya fujo kwa Vijana hao wa JKT wamehojiwa na kuachiwa kwa dhamana.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here