RC Ayoub awataka wananchi na waumini wa Dini zote kudumisha amani - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 16 December 2019

RC Ayoub awataka wananchi na waumini wa Dini zote kudumisha amani




Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Ayoub Mohamed Mahmoud amewataka wananchi ndani ya Mkoa huo kuhakikisha wanadumisha amani na utulivu uliopo Nchini.
Pia amewataka  muumini wa Dini zote kuliombea taifa kuwa salama na kupiga hatua mbali mbali za kimaendeleo.
Wito huo ameutoa wakati alipokuwa akifungua kongamano la kuiombea amani nchi lililofanyika katika kanisa la Pentercost celebration fellowship lililopo Kidimni Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema wananchi wanawajibu Mkubwa wa kuhakikisha wanadumisha amani na utulivu utulipo nchini unadumu ili kila mmoja aishi kwa amani na usalama lakini waumini wa dini mbali mbali kupata fursa ya kuwabudu ipasavyo.
Alisema Serikali ya Mkoa wa kusin Unguja itahakikisha inalinda na kudumisha amani na utulivu uliopo nchini unadumishwa.
Alisema  mbali ya serikali ya mkoa wake kutekeleza majukumu yao kupitia vyombo vya ulinzi na usalama wananchi pia wana wajibu wa kuweka ulinzi wa kiroho kwa maomba ya kuliombea taifa amani huku akisema ulinzi huo wa kiroho ukitumika vizuri basi taifa litaendelea kuwa salama.
Aidha RC Ayoub aliwataka  waumini wa dini ya mbali mbali ikiwemo uislamu na wakristo pamoja na  wananchi wote kutunza amani iliyopo kwani uwepo wa amani hiyo kumelifanya taifa lizidi kupiga hatua katika masuala mbalimbali.
Kwa upande mwingine mkuu wa mkoa huyo aliwataka  waumini hao kufanya maombi zaidi ili mungu analiondoa suala zima la udhalilishaji kwani imekuwa ni janga kubwa kwa taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kati Bi, Hamida Mussa Khamis amesema serikali itaendelea kushirikiana na viongoza na waumini wa kanisa hilo ili kuhakikisha lengo la Serikali la kuhakikisha amani ya nchi inakuwa endelevu.
Nae Mratibu wa maombi wa Mkoa wa Kusini Mchungaji, Edward Lenjima amesema lengo la kuanzisha kongamano hilo ni kuhakikisha wanaliombea taifa kuwa katika hali ya amani pamoja na kukingwa na majanga yanayolikumba taifa ikiwemo udhalilishaji wa kijinsia.
Miongoni mwa madhehebu ya kikikristo yaliyohudhuria katika kongamano hilo  la pili ni pamoja na Pentakost, KKKT, Moravian na Anglikan

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here