Waziri wa Viwanda na Biashara atoa agizo kwa Watumishi wa Wizara yake - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 16 December 2019

Waziri wa Viwanda na Biashara atoa agizo kwa Watumishi wa Wizara yake


Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amewaagiza Watumishi wa Wizara yake na Taasisi zake kuhakikisha wanasoma hotuba aliyoitoa aliyoitoa Rais Magufuli akiwa Mwanza.
Waziri Bashungwa kupitia ukurasa wake wa Kijamii ameandika; Ninamuagiza kila mtumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Taasisi zake kuhakikisha anasoma hotuba aliyotoa Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ya tarehe 12, Disemba 2019 kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya taifa (HKT) ya CCM uliofanyika mjini Mwanza. "
"Hotuba imesheheni dira, fikra na maono ambayo utekelezaji wake utaleta mageuzi makubwa ya uchumi na maendeleo ya nchi yetu na wanachi wake kufikia mwaka 2030."
"Kwa muktadha huo, Wizara inafanya zoezi la kuhakikisha sera na mipango mikakati yake yote inafanyiwa mapitio ili kuongeza weledi na wigo wa Wizara kuendelea kuratibu suala zima la ujenzi wa uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda. Tanzania ya viwanda inazidi kuonekana."
"Watanzania Tumemuelewa Rais wetu Magufuli, vision na political leadership yake ya kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini. Watanzania tumeamua kutokurudi nyuma. Mashambani, viwandani, wafanyakazi, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara, wajasiriamali tuchape kazi. Tushike neno tutende neno ili mageuzi haya yalete heri kwenye kila kaya nchini."

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here