Faida ya kujitibu kutokana na kitunguu maji - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

KABATA2

Monday, 13 January 2020

Faida ya kujitibu kutokana na kitunguu maji

KITUNGUU MAJI ni aina ya mboga ya yungiyungi. Ni mboga yenye harufu kali inayochangamsha. Anaeikitumia kitunguu maji ajihadhari kukitumia baada ya kukihifadhi kikiwa kimekatwakatwa, kwasababu hufanya oksaidi (oxide) na huwa kiini chenye sumu. Kwa hivyo yatakiwa kitumiwe kikiwa fresh.Imethibitiswa kisayansi kuwa juisi yake huuwa vijidudu vya kamasi  na vya kifua-kikuu, huuwa baada tu ya kunusa moshi wake.Nchi mashuhuri duniani katika upandaji wa kitunguumaji ni Misri (Egypt).Katika gazeti moja huko Ufaransa liitwalo “Everything” (Kila kitu) limeelezea kuwa daktari mmoja aliwatibu wagonjwa kwa kuwapiga sindano (ya kitunguumaji) wagonjwa wengi waliokuwa na saratani (cancer) na akapata matokea mazuri.Viini vyenye athari nzuri katika kitunguu maji ni Vitamin C (antiseptic) inayozuia kukua kwa bakteria (bacteria) kwenye jeraha, ngozi n.k pia hutia nishati homoni (hormones) wa nguvu za kiume, kiini cha insulini (insuline, itumikayo kutibu wagonjwa wa kisukari). Kwa hivyo kitunguu maji ni katika dawa yenye kuwatibu wagonjwa wa kisukari, ndani yake mnapatikana salfa, chuma na vitamini zinazotia nguvu mishipa. Vilevile hupatikana viini vyenye kukojoza, kutoa safura na vyenye kutia nishati moyo pamoja na mzunguko wa damu mwilini.Pia imethibitishwa kuwa katika kitunguu maji muna vijiuasumu vyenye nguvu zaidi kuliko penesilini (penicillin) kwahivyo hupoza kifua kikuu, kaswende (syphillis) na kisonono (gonorrhea), na huua aina ya vijidudu vingi vya hatari.Pamoja na kuwa tunaamini kuwa maisha ya mwanaadam yote yamo katika mikono ya Allah S.W, lakini imethibitishwa kuwa wale watumiaji wa vitunguu maji zaidi huwa na umri mrefu pia huepukana na maradhi ya saratani na kifua kikuu.Mwandishi wa kitabu cha tiba zinazotokana na kitunguu maji yeye amekiita kitunguu maji ni ” mpira wa dhahabu” kwakuwa ndani yake muna manufaa mengi yenye utajiri wa afya. Kutakasika ni kwa Allah mwenye kuneemesha peke yake.MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUUMAJIPumu:Changanya juisi ya kitunguu maji na asali halafu kunywa kiasi cha kikombe kimoja, asubuhi na jioni. Endelea hivyo kwa muda wa mwezi mmoja.Uvimbe wa pafu (Pneumonia):Weka kibandiko cha kitunguu maji juu ya kifua na mgongo pamoja na kufunga kwa kitambaa, fanya hivyo kila siku kabla ya kulala.Saratani (Cancer):Kausha maganda ya kitunguumaji kwenye jua, yasage na kiasi halafu yakande katika asali na chukua na uchanganye katika juisi ya karoti (carrot) na unywe kiasi ya kijiko kimoja kwa muda wa mwezi mzima mfululizo, na baadae uvute moshi wa kitunguu maji kabla ya kulala.Mvilio wa damu (Bruise):Changanya juisi ya kitunguu maji pamoja na kiasi cha mafuta ya kafuri, sugua mahala pa mvilio asubuhi na jioni.Majipu:Saga kitunguu maji na kikange katika mafuta ya zaituni bila ya kuwa rangi ya manjano, paka kama marhamu na funga bendeji juu yake. Kila siku ukibadilisha pamoja na kusafisha utokaji wa usaha umalizike, halafu utakuwa ukitumia habasouda.Chunusi:Chukua kitunguu maji kisha ukisage, halafu ukikande katika unga wa ngano nzima, changanya na yai pamoja na mafuta ya simsim(ufuta) na upake usoni asubuhi na jioni pamoja na kula kitunguu kwa sana.Ukurutu (Eczema):Chukua juisi ya kitunguu na nanaa (mint) vipimo sawa, tengeneza kama krimu (cream) na ujipake baadae pangusa ukurutu kwa maji ya siki nyepesi, rudia kila siku pamoja na kujiepusha na kila kinachochea hisia. Kula matunda, mboga na asali kwa wingi.Saratani ya ngozi:Chukua juisi ya kitunguu maji, uwatu uliosagwa na salfa manjano kiasi cha robo kijiko kidogo; tengeneza marhamu jipake kila siku. Baada ya kuosha jioni jipake mafuta ya zetuni endelea hivyo kwa muda wa wiki.Mgonjwa wa figo na vijiwe:Chukua kitunguu bila kukichambua, tia mbegu ya tende baada ya kuichoma kama vile buni na kuisaga; halafu kila siku kula kimoja kula kimoja kwa muda wa wiki.Kikohozi kwa wakubwa na wadogo:Saga kitunguu kitie ndani ya kikombe cha asali; iwache kwa muda wa masaa matatu (3) kisha uisafishe. Kula kiasi cha kijiko kimoja kila baada ya chakula.Kisukari (Diabetes):Kila siku kula kitunguu. Sukari itashuka na baadae kula mzizi wa kabichi (cabbage).Kikohozi:Chemsha maji ya kitunguu maji na asali kunywa kijiko kimoja kila baada ya kula na weka kibandiko cha kitunguu maji juu ya kifua na majani yake kwa bendeji kabla ya kulala.Kufungua choo:Chambua kitunguu, tia katika maziwa na kunywa.Kutia nguvu na nishati:Choma kitunguu pamoja na maganda yake halafu kichambue na ukikande katika asali na samli, weka katika mkate wa ngano nzima kama vile sandwich. Kula wakati wa chakula cha asubuhi na unywe maziwa nusu lita.Kupunguza uzito:Kwa anaetaka kufurahi mwili wake uwe mzuri na mwepesi, kuyayusha mafuta na kuondoa kitambi na mwili tepwetepwe miongoni mwa wanaume na wanawake basi afwate hivi:1. Kila siku kunywa maji ya kitunguu maji kiasi cha kijiko kimoja kidogo unaweza kuchanganya katika juisi ya matunda ukanywa.2. Soma sana katika masaa ya mwisho wa usiku na kukizingatia ukisomacho (ukisoma Quraan utapata faida 2 kwa wakati mmoja, moja ya hapa duniani na moja ya huko tunapokwenda akhera) pia usile chakula cha usiku isipokuwa maziwa ya mgando kikombe kimoja, au matunda.3. Tembea sana na kufanya mazoezi kwa wingi.MAKALA hii imeandikwa kwa msaada wa mtandao

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad