KWANINI UNAPATA CHOO KIGUMU NA KWASHIDA? - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

KABATA2

Monday, 13 January 2020

KWANINI UNAPATA CHOO KIGUMU NA KWASHIDA?

atizo hili tunaliita Constipation ,tatizo hili linalotokea pale mtu anapopata hajakubwa (choo) Ngumu na kidogo mara kwa mara.Kwa kawaida mida ya mtu kupata choo inatofautiana, kuna wengine hupata choo mara tatu kwa siku, wengine mara moja au mara mbili kwa wiki lakini endapo mtu itamchukua zaidi ya siku tatu bila kupata choo huo ni muda mrefu sana, choo huwa kigumu na hutoka (kujisaidia) kwa shida.Mtu husemekana kua na tatizo la Constipation endapo tu atakua na mambo ya fuatayo mawili au zaidi ya mawili kwa muda wa miezi miwili:¤ Kujikakamua kwa nguvu sana wakati wa kujisaidia(kunya).¤ kupata choo kigumu sana mara kwa mara kinachoambatana na damudamu.¤ kutokumaliza haja mara nyingi (yaani ukijisaidia choo hakitoki chote, unahisi bado kimebaki ndani lakini ukikisukuma hakitoki).¤ kupata choo kidogo na kigumu tena mara moja au mbili kwa wiki.¤ Choo kua na damu (au ukijisafisha/chamba una ona damu kwenye Toilet paper).¤ Mgongo na kiuno kukaza (back pains).SABABU ZINAZOLETEKEZA TATIZO LA CONSTIPATION:¤ Kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.¤ Kutokutumia vyakua aina yakambakamba (fibers).¤ kutokupata mlo kamili,¤ kukaa au kusafiri umbali mrefu mara kwa mara.¤ kutokufanya mazoezi au kazi za mwili(kazi za kutumia nguvu).¤ Utumiaji wa vyakula vya makopo au viwandani mara kwa mara (vyakula vya kusindika).¤ Msongo wa mawazo.¤ Kujizuia kwenda haja kubwa (kujisaidia) , ambapo unaweza sababisha tatizo lingine hatari sana linaitwa (Hemmorhoids) bawasili( uvimbe katika njia ya haja kubwa). Â¤ Upungufu wa homoni (Hypothyroidism) mara nyingi kwa watu wazima.¤ Utumiaji wa Vilainishi vya haja kubwa (Stool softeners) kwa muda mrefu.¤ Matatizo ya mfumo wa usambazaji taarifa mwilini (Neurological conditions) kama vile mwili kutetemeka (parkinson's Disease) ,hasa kwa wazee na wanyanyua vyuma au wapiiganaji.¤ Utumiaji kwa wingi dawa za kupunguza acid au gesi tumboni zenye Calcium au Aluminium.¤ Mimba (kwa wanawake wajawazito).¤ Kansa ya Utumbo mpana (Colon Cancer).UCHUNGUZI WA TATIZO LA CONSTIPATION:Watu wengi hupuuzia kuchunguza tatizo hili hatima yake tatizo huongezeka na kusababisha tatizo lingine hatari sana hemmorrhoids).Hivyo basi mgonjwa huchunguzwa kwa:¤ Kupimwa damu ili kujua kama homoni hazija balansi (Hormonal imbalance).¤ mgonjwa huchunguzwa kwa kutumia kifaa maalumu chenye mwanga (Colonoscopy) ambacho huingizwa kwenye njia ya haja kubwa ili kuonesha kama kuna tatizo kwenye utumbo mpana.¤ Physical examinition, Doctor anamwingizia kidole mgonjwa kwenye njia ya haja kubwa ili kuchunguza kama kuna tatizo kwa ndani.TIBA YA TATIZO LA CONSTIPATION:¤ Mgonjwa anatakiwa kutumia vyakula aina ya kambakamba kwa wingi.¤ kutumia maji mengi kwa siku,¤ kujisaidia mara moja bila kujibana pindi ajisikiapo kujisaidia (kunya).¤ kufanya mazoezi ya mwili.¤ pindi tatizo linapozidi kua kubwa mgonjwa hupewa dawa kama Atimiza na Linzess kwaajili ya matumizi ya muda mrefu.Hili ni tatizo linalosumbua watu wengi sana katika jamii,humkosesha mtu amani kabisa.hasa pale linapoelekea kutengeneza bawasiri.Tiba ya tatizo hili ni dawa aina ya Ginsenoside na Aloe .Ginsenoside,(antitumor) huondoa uvimbe wowote ulio katika mfumo wa chakula,ikiwa na maana kua endapo kama kutakua na dalili za bawasili (uvimbe kwenye hajakubwa) wakati,Aloe (relaxant),hufanya kazi ya kurekebisha mfumo mzima wa mmeng'enyo wa chakula na kumfanya mtu apate choo kwa ulaini na bila maumivu.Dawa hizi zote mbili ni dawa asili zenye nguvu (strength) ya 300mg.hivyo utavitumia vidonge hivi asili kwa muda wa siku 15 . na kisha hali yako kutengamaa.Ginsenoside, ni dawa (TCM) imezalishwa kutokana na mizizi ya mimea,wakati Aloe ni kirutubisho kilichozalishwa kwa matunda na majani ya mimea.Dawa hizi ni matokeo baada ya kupembuliwa kwa umakini kile kiini tiba (extraction of Active Pharmaceutical Ingridient) na kuwekwa katika mfumo salama na rahisi kwa matumizi ya mgonjwa.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad