Kanuni za kilimo bora cha mahindi - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

KABATA2

Monday, 13 January 2020

Kanuni za kilimo bora cha mahindi



C8ukqZVWAAApYI4Mahindi ni zao muhimu linalo limwa katika maeneo ya kitropiki. Pia zao hili hulimwa katika udongo wenye uchachu pH 6-6.5. lakini pia hustawi zaidi kwenye maeneo yenye mwinuko wa 2500.
Kanuni ya kwanza – kutayarisha shamba mapemaTayarisha shamba la mahindi mara tu baada ya kuvuna mazao ya msimu uliopita.Mahindi hustawi sehemu yenye udongo wenye rutuba na usiosimamisha maji.Moto usitumike wakati wa kuandaa shamba.
Faida ya kuandaa shamba mapemaBaada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi kwa kutumia jembe lolote.Masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema.Hupunguza magugu.Hupunguza wadudu waharibifu.
Kanuni ya pili ; kujua wakati wa kupanda mbegu sahambani.Wakati wa kupanda hutatanisha kwani mvua haitabiriki, Kama mvua hunyesha nyakati na majira yale yale ya mwaka basi kalenda ifuatayo inaonyesha tahere za kupanda zao la mahindi katika eneo lako.
Mbeya na maeneo ya jirani, mwanzoni mwa mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni.Morogoro na maeneo ya jirani, Mwezi Januari katikati hadi Februari katikatiIringa na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Desemba mwishoniSongea na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Januari mwanzoni.
Kupanda mahindi mapema ni muhimu kwani uwezekano wa kuvuna mazao mengi ni mkubwa. Kwa mashamba makubwa makubwa sana wakati wa kupanda uwe wiki moja kabla ya mvua kuanza kunyesha na isizidi wiki mbili kabla ya mvua.
Isiwe mapema zaidi kwani mbegu zitaharibiwa na joto kati ya udongoni wadudu, panya, ndege na wanyama wengineo.
Faida za kupanda mapemaMahindi yanapata mvua ya kutosha hadi kukomaa.Magonjwa kama yale ya ya majani (streak ugonjwa wa milia) hayatatokea au yatakuwa kidogo.Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na mahindi yastawi vizuri.Kanuni ya tatu kuchagua mbegu boraMbegu bora ni zile zilizo zalishwa kitaalamu.Ni safi hazijabunguliwa na wadudu.Huzaa mazao mengi.Hustahimili magonjwa.
Aina za mbeguMbegu aina ya chotara (hybrid)Aina ya ndugu moja (synthetic)Mbegu aina ya compositeMbegu za kisasa zikitumiwa vizuri katika vizuri katika misingi ya kilimo zina uwezo wa kuzaa magunia 50-80 au tani 5.5 – 7.5 kwa hekta moja au umi kwa hekari.
Mapendekezo ya mbegu za kupandaKuna mbegu nyingi za kisasa zilizoko kwenye soko mfano wa SIDCO ,PANNAR, CHOTARA, kutoka KENYA n.k Ni vyema kufuata ushauriwa wataalamu wa kilimo.
Kanuni ya nne kupandaIdadi ya mimea katika eneo ni muhimu kwani ikazidiMazao hupungua.Mmea huangushwa na upepoMabua mengi hayazai.Idadi ya mimea nayo ikipungua kwenya eneo husababishwa mavuno kupungua jambo la kufanya ni kupanda mbegu katika nafasi sahihi zilizoshauriwa na wataalamu.
Kiasi cha kupandaMbegu za mahindi huhifadhiwa kwa dawa kali(sumu Kiasi cha kilo 20(ishirini) za mbegu kinatosha kupanda hekari moja., (Hii hutegemea na aina ya mbegu)
Nafasi za kupanda.75cm x 30cm75cm x 60cm90cm x 25cm90cm x 50cm
Kanuni ya tano; kutumia mboleaMahindi hustawi na kuzaa vizuri iwapo yatapatiwa mbolea pamoja na matunzo mengine ya kilimo bora. Ukipanda mbegu bora bila kutumia mbolea ni kazi bure.
Kuna aina mbili kuu za mboleaMbolea za asili mfano; samadi,mboji na majani mabichi,mbolea hizi hua na virutubisho vya kutosha ambavyo havijulikani vipo kwa kipimo kiasi gani.
Mbolea za viwandani, hizi hua na virutubisho vya kutosha na vipimo hujulikana, hii inasaidia kujua ni kiasi gani kitumike kwa kipindi gani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad